Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Roho ya Wesley Ilichangamka Kiajabu

  Wesley aliporudi Uingereza alikuwa na ufahamu kamili wa Biblia na imani ya kweli, kwa kuwa alifundishwa na watu wa Moravian, katika makutano wa watu wa Moravia, uliokuwa London, palisomwa andiko la Luther. Wesley aliposikiliza, imani iliwaka moyoni mwake. Alisema, “Nilijisikia kuchangamka kwa ajabu, nilijisikia kumtumaini Kristo, Kristo mwenyewe tu ndiye aletaye wokovu. Nikajisikia kuwa na hakika ya kusamehewa dhambi zangu, kwamba nimeokolewa na sheria na adhabu ya kifo”TU 119.3

  Sasa akajua kuwa neema ya Mungu aliyokuwa akiitafuta kwa njia ya maombi ya kufunga na kujitesa kwa kila hali, ilikuwa “kipawa cha bure”. Moyo wake ukajaa, naye akawa na hamu ya kutangaza neema ya Mungu ya bure kila mahali. Akasema, “Nikatazama ulimwengu wote kuwa mtaa wangu wa kazi. Kila mahali pakaonekana kuwa pananipasa kupahubiri Injili”TU 119.4

  Aliendelea na maisha yake ya kujikana na kujinyima, lakini sasa si kama tegemeo la wokovu, bali kama matokeo ya imani, Wala si kama shina, bali matawi ya utakatifu. Neema ya kristo itadhihirishwa kwa njia ya utii, maisha ya Wesley yalitolewa kuhubiri Injili aliyoipokea, ambayo ni Roho Mtakatifu, uzao matunda maishani yaimarishayo mfano wa Kristo.TU 120.1

  Whitefield na Wesley walidharauliwa na kuitwa wafuasi wa “Medhodist” na wanafunzi wenzao, jina ambalo kwa wakati wa sasa ni la heshima. Roho Mtakatifu akawaongoza wahubiri Kristo tu aliyesulubishwa. Watu wengi waliongoka kwa mahubiri hayo. Basi ulikuwa lazima waamini hawa kama kondoo wa Mungu walindwe na mbwa mwitu. Wesley hakuwa na wazo la kuanzisha dhehebu jipya; ila aliwaunga Methodist.TU 120.2

  Majaribu na matatizo ya siri yaliwapata wahubiri hawa kutoka kwa kanisa mama. Walakini ukweli huingia popote hata kama milango imefungwa. Hata wakuu waliamshwa wakatoka usingizini na kuwa wahubiri hodari katika mitaa yao.TU 120.3

  Siku hizo za Weslye watu wenye vipawa mbalimbali hawakupatana katika mafundisho. Kukubaliana baina ya whitefield na Weslye wakati fulani kulileta tisho la kufarakana lakini basi walijifunza upole wa Kristo, na uvumilivu wa kusutana na kufarakana, wakati makosa ya wazi yalikuwa yameanza kila mahali.TU 120.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents