Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Katika Kuitetea Sheria Ya Mungu

  Wesley akijibu hoja ya kwamba eti Yesu alipokufa aliifuta sheria ya Mungu pamoja na sheria ya Musa, alisema, “Sheria ya Mungu ambayo ni amri kumi, na iliyotukuzwa na manabiii, haikufutwa kamwe. Sheria hii haivunjiki kabisa nayo husimama mbinguni kama shahidi mwaminifu”TU 122.2

  Wesley aliueleza mwungano wa sheria na Injili. Kwa upande mwingine, sheria hutuelekeza kwa Injili, nayo ni njia ambayo sisi tunapitia kuendea Injili. Na kwa upande mwingine Injili daima hutuweka katika utimilifu wa sheria. Kwa mfano, sheria hututaka tumpende Mungu, tuwapende wenzetu, tuwe wapole, na wanyenyekevu na watakatifu. Nasi hujionakuwa hatuwezi kuwa kama sheria inavyotaka tuwe, lakini tunaona ahadi ya Mungu ya kutuwezesha tuwe na upendo, na kuwa na upole na unyenyekevu na utakatifu. Nasi tunaishikilia Injili ambayo ni habari njema. Haki ya sheria hutimizwa ndani yetu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.TU 122.3

  Wesley alisema: “Maadui wakubwa wa Injili ni wale wanaofundisha kuwa sheria haina haja kushikwa. Kuvunja hata kipande kidogo tu, na kujidai kuwa wana wa Mungu huwa na heshima kama ile ya Yuda aliyokuwa nayo kwa Kristo akijidai kumsalimu. ‘Salam Bwana, na kumbusu’ ‘Ni usaliti’ kuzungumza juu ya damu yake na kuiondoa taji yake kuangaza kwa sehemu ya sheria yake kwa ujanja kueneza Injili yake ni usaliti.”TU 122.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents