Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uadui Dhidi Ya Kristo

  “Pale Bwana wetu aliposulubishwa”. Jambo hili lilitimizwa na Ufaransa pia. Hakuna nchi iliyoupinga ukweli kwa ukatili sana kuliko Ufaransa. Katika mateso yaliyowapata wakristo walioamini Injili, Ufaransa, ilimsulibisha kristo kwa njia ya wanafunzi wake.TU 126.4

  Karne baada ya karne damu za watakatifu zilizidi kumwagika. Wakati watu wa Waldenses walipouawa katika milima ya Piedmont kwa ajili ya Kristo, mambo yale yalitokea katika Ufaransa kwa wa Albigenes. Wafuasi wa matengenezo ya kanisa waliteswa na kuuawa kikatili mno. Mfalme na wakuu wanawake waheshimiwa na vijana walishibisha macho yao kwa kuyaona mateso ya ukatili mkubwa yaliyowafikia wafia dini wa Yesu. Mashujaa wale wahuguenots walimwaga damu zao katika vita vingi vigumu, walipokuwa wakiwindwa kama wanyama pori.TU 126.5

  Wazao wachache wa wakristo wa zamani waliokuwa wangali Ufaransa katika karne ya kumi na nane, waliokuwa wakijificha katika milima ya kusini, waliendelea kushikilia imani ya baba zao. Walivutwa wakitiwa katika kazi za kitumwa maisha yao yote. Waliokuwa na akili na uwezo katika Ufaransa walikamatwa na kufungwa, na kuteswa kikatili mno, wakiwa pamoja na wanyang'anyi na wauaji. Wengine walipigwa na risasi wakafa walipokuwa wakipiga magoti kusali. Nchi yao iliachwa ukiwa kwa upanga na mashoka. “Ilifanywa jangwa moja kubwa lenye majonzi”TU 127.1

  “Maovu haya yalifanyika kisheria siyo katika nyakati za giza bali katika nyakati za maendeleo, wakati wa mfalme Louis XIV, Elimu ya sayansi ilikuwa inaendeshwa, sheria halali za mahakama zilikuwa zikitungwa na watu wenye busara na wasomi ambazo zilisakama hali nzuri ya wema na unyenyekevu na upendo”.TU 127.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents