Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Maasi Makuu Ya Kutisha.

  Lakini matendo maovu mno ya kishetani yaliyotendeka katika karne za kutisha ni yale mauaji ya St. Bartholomew. Mfalme wa ufaransa akihimizwa na makasisi wa Rumi aliunga mkono maazimio hayo maovu. Kengele iliyopigwa usiku wa manane ndiyo iliyokuwa alama ya machinjo yake.TU 127.3

  Waprotestanti kwa maelfu walikuwa wamelala manjumbani mwao huku wakimheshimu mfalme wao, walikokotwa na kupelekwa machinjioni ili wakauawe.TU 127.4

  Mauaji yaliendelea muda wa siku saba katika mji wa Paris. Kwa amri ya mfalme mauaji yaliendelea na kufika hata katika miji mingine, ambako Waprotestanti walikutwa, watu wakuu na wakulima watu wazima na watoto, akina mama na vijana wamechinjwa wote pamoja. Katika Ufaransa watu kiasi cha 70,000 walipotea.TU 127.5

  “Habari ya mauaji haya ilipofika Rumi, shangwe ya waongozi wa kanisa ilizidi mno. Kadinali wa Lorraine alimtuza mleta habari taji maelfu. Kasisi wa Angelo aliposikia alishangilia sana, kengele za shangwe zikapigwa kwa kila mnara wa kanisa. Mioto ikiwashwa ambayo iliuangaza usiku ukawa kama mchana; na Gregory XIII akifuatana na makasisi, makadinali na wakuu wengine waliandamana mpaka katika kansia la St. Louis ambako kadinali wa Lorraine aliimba. Chuma kiligongwa ili kuadhimisha mauaji hayo…. Kasisi wa Kifaransa aliinena siku hiyo kuwa siku iliyojaa furaha na shangwe, ambapo papa alipopata habari hizo alikwenda ikulu kutoa shukrani zake kwa Mungu na kwa mfalme Louis”TU 127.6

  Roho ile ile iliyoongoza kwenye mauaji ya St. Bartholomew ndiyo iliyoongoza katika mapinduzi. Yesu Kristo alitajwa kuwa mlaghai na mdanganyifu. Kwa hiyo usemi wa Wafaransa wakafiri ulikuwa: “Mwangamize huyu movu” yani Kristo. Kufuru na ufisadi vilienda bega kwa bega. Kwa njia hii walimheshimu na kumtukuza shetani na Yesu mwenye tabia safi ya kweli, mwenye upendo “alisulubishwa”TU 128.1

  Mnyama aliyetoka kuzimu alifanya vita nao, na kuwashinda ufunuo 11:10. Roho ya ukafiri iliyotawala Ufaransa wakati wa mapinduzi na utawala wa kitisho, ilifanya vita na Mungu na Neno lake. Ibada ya kumwabudu Mungu ilipigwa marufuku na bunge la taifa. Biblia zilikusanywa na kuchomwa moto hadharani. Shule za biblia zilipigwa marufuku. Siku ya badala yake ikawekwa kila siku ya kumi ya juma iwe ndiyo siku ya kupumzika. Ubatizo na meza ya Bwana vilikatazwa. Matangazo yakawekwa pote penye makaburi yakisema, kuwa kifo ni cha milele, hakuna ufufuo.TU 128.2

  Ibada zote za kidini zilipigwa marufuku, ila tu siku ya kuadhimisha uhuru. Askofu halali wa Paris aliletwa mbele …. Atangaze wazi hadharani kuwa dini aliyokuwa akifundisha kwa miaka mingi ilikuwa upuuzi tu, wala haina msingi kihistoria wala kimaandiko matakatifu. Alikana dhahiri kwamba hakuna Mungu, ambaye alikuwa amejitoa kuabudu miaka yote hii. “Nao wakaao juu ya nchi walifurahi juu yao na kushangilia. Nao walipelekeana zawadi wao kwa wao juu ya nchi” Ufunuo 11:10. Wakafiri wa Ufaransa wamewanyamazisha mashahidi wawili wa Mungu. Neno la Mungu likaanguka limekufa katika barabara za ufaransa, na wale waliomchukia Mungu walishangilia. Watu wakamkana dhahiri mfalme wa mbinguni.TU 128.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents