Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mungu Alitawala Mambo

  Wakati mkono wa Mungu ulipoonekana ukiwaonyesha nchi iliyoko ng'ambo ya bahari, ambayo itakuwa makao yao ya amani na uhuru, itakayokuwa urithi wa watoto wao wenye uhuru wa dini, walifuata maongozi hayo. Mateso na kufukuzwa vilifungua njia ya uhuru.TU 136.6

  Wapuritani walipolazimika kuachana na kanisa la Kiingereza, walijiunga wenyewe kwa kiapo kwamba watakuwa “watu huru” watakaofuata njia ya Bwana, kadiri walivyofunuliwa katika Maandiko Matakatifu. Hapa ndipo palikuwa kanuni hasa ya Kiprotestanti. Wakiwa na maazimo hao wasafiri hawa waliondoka Uholanzi kwenda kutafuta makao mapya katika nchi mpya. Mchungaji wao aitwaye John Robinson, katika ujumbe wake wa kwaheri kwa wakimbizi hawa alisema:TU 136.7

  “Nawaagiza mbele za Mungu na mbele za Malaika zake watakatifu kuwa msinifuate zaidi ya ninavyomfuata Kristo. Ikiwa Mungu atawafunulia jambo jipya kwa njia yake mwenyewe, lipokeeni kwa moyo jinsi mlivyopokea mambo katika huduma yangu; maana nina matumaini kwamba Bwana anazo kweli nyingi ambazo atazifunua zaidi katika Neno lake Takatifu.”TU 137.1

  “Kwa upande wangu, sitaombolezea hali ya makanisa ya matengenezo kiasi cha kutosha…. Ambao kwa wakati huu hawatakuwa kama vyombo vya matengenezo ya kanisa. Walutheri hawawezi kuvutika kuwa namna nyingine zaidi ya ile ya Luther aliyoona, na wafuasi wa Calvin, mnaona, wanasimama pale walipoachwa na mtu huyu wa Mungu, ambaye hakuona mambo yote vile vile,... Ingawa katika nyakati zao walikuwa huru waking'aa na hata hivyo hakufunuliwa mambo ya Mungu yote. Kama wangekuwa wangali hai leo wangekuwa tayari kupokea mambo zaidi kama walivyokuwa hapo mwanzo”TU 137.2

  “Kumbukeni ahadi zenu na agano lenu na Mungu na mapatano yenu ninyi kwa ninyi, kwamba mtakuwa tayari kupokea ukweli wote utakaofunuliwa katika Neno lake. Walakini nawatahadharisha kwamba, chochote mpokeacho kuwa ni kweli, kichunguzeni na kukipima kwa njia ya Neno takatifu la Biblia, mkilinganisha andiko na andiko kabla hamjalipokea, maana haiwezekani kuwa ukristo utoke katika giza la kumpinga Kristo, ujuzi wa kweli uutajidhihirisha”.TU 137.3

  Hamu ya uhuru wa dhamiri iliwachochea wasafiri hao kuvuka bahari, wakivumilia shida, na kupambana na matatizo ya jangwani ili kuweka msingi halisi wa taifa. Hata hivyo wasafiri hao wahakufahamu kanuni za uhuru wa dini. Uhuru ambao walijitolea kuupata, hawakuwa tayari kuuachia. Makosa ya upapa ambayo yalikuwa ndiyo shina la uovu wao, yalikuwa kwamba, mafundisho ya Mungu anataka kanisa litawale dhamiri za watu, na kwamba mpingaji yeyote aadhibiwe. Watengenezaji hawakuachana na kosa hilo la Rumi la kutovumilia. Giza nene la makosa ambayo Rumi imeanzisha halikufutika kabisa.TU 137.4

  Aina ya utawala wa kanisa ulianzishwa na wananchi, mahakama yalipewa uwezo wa kuwaadhibu wapingaji wa mambo ya kidini. Kwa hiyo kanisa lilikuwa na uwezo kama ule wa serikali. Hali hii ilileta mateso.TU 137.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents