Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Roger Williams

  Roger Williams alifika nchi mpya ili kuufurahia uhuru wa dini sawa kama wasafiri wengine waliomtangulia. Lakini aliona kuwa uhuru huu ni haki ya kudumu kwa wote hilo lilikuwa jambo ambalo watu wengi walikuwa hawajaliona. Williams alikuwa mtafuta ukweli hasa. Alikuwa mkristo wa kwanza zamani hizi aliyebuni serikali ya kiraia yenye misingi ya uhuru wa “dhamiri” Alisema, hakimu, au watu wanaweza kuamua mambo yampasayo mtu amtendee mwenzake; lakini wanapojaribu kuingilia mambo yampasayo mtu amtendee Mungu, hapo huwa wamepotoka kabisa, wala hakuna usalama. Maana ni dhahiri kuwa kama hakimu akiwa na uwezo, anaweza kutunga mawazo, au imani kuhusu leo na kutunga wafalme wengi; na ilivyokuwa ikifanywa na mapapa na mabaraza ya kanisa la Rumi.TU 138.1

  Mahudhurio katika kanisa, ilitolewa adhabu ya fani au kifungo, kama mtu hakufuata kanuni za kanisa sawasawa. Williams alisema, “Kuwalazimisha watu wasiokuwa wa dhehebu moja nawe, ili kufuata dhehebu lako ni kuvunja uhuru wa dhamira ya mtu, na kumlazimisha mtu aabudu bila dhamira yake, ambayo ni unafiki mtupu …. Mtu yeyote asilazimishwe kuabudu bila hiari yake”TU 138.2

  Roger Williams aliheshimiwa, walakini msisitizo wake kuhusu uhuru wa dini haukupendwa. Ili kuepuka asikamate ililazimika kutoroka wakati wa baridi kali na dhoruba, akakimbilia katika msitu mnene. Asema, “Kwa muda wa majuma kumi na manne nilihangaika msituni katika baridi bila kula wala kulala” Lakini, kunguru walinilisha jangwani, na mvungu wa mti ulikuwa maficho yangu. Aliendelea na mahangaiko yake katika barafu msituni mpaka kafika kwa mhindi mmoja aliyemhurumia na kufanya naye urafiki, akamtunza.TU 138.3

  Aliweka msingi wa kwanza wa serikali ya kisasa ambayo hutambua uhuru halisi ya kwamba kila mtu budi amwabudu Mungu kwa hiari ya moyo wake, sio kulazimishwa. Kisiwa kiliendelea na kustawi mpaka kanuni zake za uhuru wa dini na wa mtu binafsi zikawa msingi halisi wa serikali ya Marekani.TU 138.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents