Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mkataba wa Uhuru.

  Tamko la tangazo la uhuru wa Marekani lilisema, “Tunashikilia kweli hizi ziwe mashahidi, ya kwamba, watu wote waliumbwa kwa usawa; kwamba kila mtu alipewa na Muumba wake haki fulani ya kudumu; baadhi ya haki hizi ni uzima (maisha), uhuru, na starehe (furaha). Katiba inatoa haki ya hiari ya kila mtu, yaani kutoingilia dhamira ya mtu. Bunge halitatunga sheria yoyote ikiegemea upande wa dini, au ikiunga mkono dini yoyote, au kukataza dini yoyote. Waundaji wa katiba walielewa kanuni za utu, kwamba uhusiano na mtu na Mungu wake hauingiliwi na sheia yo yote, na hata ya kwamba hiari yake ni ya kudumu haiingiliwi na chochote.”TU 139.1

  Habari zikaenea Ulaya nzima kuwa nchi ya Marekani kila mtu yu huru kufuatilia matunda ya kazi yake bila kuingiliwa; na kila mtu hufuata jinsi dhamira yake inavyomwongoza. Kwa hiyo watu maelfu wakafurika kwenda katika Nchi Mpya. Kwa muda wa miaka ishirini tangu wasafiri wa kwanza walipofika Pylymouth (1620) watu maelfu wamehamia New England (Marekani). Hawakukaa na kutapatapa, ila kila mtu alishika jembe na kulima na kupata mavuno ya kazi yake. Walivumilia upungufu wa vitu walivyoacha ulaya bila manung'uniko, wakisamadi mti wa uhuru wao kwa machozi, na kwa jasho la uso waliendelea mpaka mafaniko makubwa yakatokea.TU 139.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents