Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ukuu wa kweli wa Usalama wa Taifa.

  Kanuni za Biblia zilifundishwa nyumbani, shuleni na kanisani. Matunda yake yalionekana maishani mwa watu wakiwa waangalifu, wenye maarifa, wanyofu, wenye kiasi. Mtu alimaliza mwaka mzima bila kuona mlevi, wala mfedhuli, au kuona mtu akiombaomba barabarani. Kanuni za Bibia ndizo usalama wa kweli kwa ustawi wa taifa. Mahamio mapya yaliyokuwa na hali ya ufukara yaligeuka kuwa nchi zenye usatawi mkuu, na ulimwengu ulio na ustawi wa kanisa bila kuwa na papa, na serikali bila kuwa na mfalme.TU 139.3

  Lakini ongezeko la watu huko Marekani lilikuwa na nia tofauti na ya wale wasafiri wa kwanza waliohamia huko. Ongezeko la watu lilikuwa na nia ya kutafuta uchumi, mali ya dunia hii tu.TU 139.4

  Serikali ya mahamio, iliruhusu tu washiriki kupiga kura, kuweka wakristo tu katika madaraka. Hali hiyo ilikubaliwa ili kutunza serikali iwe na watu waaminifu. Lakini matokeo yake yakawa kuchafua kanisa. Watu wengi walijiunga na Constatine mpaka leo, jaribio la kutaka msaada wa serikali katika kuendesha mambo ya kanisa ingawa inadhaniwa kuwa ni kuvuta ulimwengu ukae kanisani, lakini ukweli ni kulivuta kanisa liende ulimwenguni.TU 139.5

  Makanisa ya Kiprotestanti ya Marekani, hata yale ya ulaya, yameshindwa kuendelea katika njia ya watengenezaji wa kwanza. Watu wengi wanafanana na Mafarisayo wa wakati wa Kristo, au Warumi siku za Martin Luther, kwamba ufedhulli vinaendelea katika imani zao. Baadaye matengenezo yalizimika polepole mpaka ikawako haja ya kuwa na makanisa ya Kirumi, wakati wa Luther. Wakati huo mawazo ya kibinadamu ndiyo yaliyoheshimiwa kuliko neno la Mungu. Watu walikoma kuchunguza Neno la Mungu, hivyo walibaki na mapokeo tu ya watu ambayo hayana msingi katika BibliaTU 140.1

  Kiburi na anasa viliingia kanisani na kuhesabiwa kuwa ni sehemu ya dini, na kanisa likaoza kabisa. Mapokeo tu ambayo yalikuwa na uharibifu yalikuwa na nguvu kanisani. Kanisa likayashikilia mapokeo hayo badala ya imani iliyokabidhiwa kwa watakatifu.TU 140.2

  Hivyo kanuni za kweli zilizowekwa na Watengenezaji zilidharauliwa na kuwekwa kando.TU 140.3

  Marejeo: TU 140.4

  J. Bown, The Pilgrim Fathers, p. 74 TU 140.5

  Martiny, Vol. 5. p. 70 TU 140.6

  D. Neal, History of Puritants Vol. 1 p. 269 TU 140.7

  Martyn, Vl. 5 p. 70-71. TU 140.8

  Bancroft, pt. 1 ch. 15 para. 2 TU 140.9

  Martyn, Vol. 5 p. 340 TU 140.10

  Bancroft, pt. 1 ch. 15 para. 2 TU 140.11

  Martyn, Vol. 5 p., 349-350 TU 140.12

  Ibid. Vol. 5 p. 354 TU 140.13

  Conresional Documents (USA), serial No. 200.TU 140.14

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents