Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  17/Ahadi Za Kurudi Kwa Kristo

  Ahadi za kurudi kwake Kristo mara ya pilli ili kukamilisha kazi kuu ya ukombozi ndio msingi wa Maandiko matakatifu. Tangu huku Edeni watu waaminifu wa Mungu amekuwa wakingoja Kristo aje na kurejesha Paradiso iliyopotea. Enoko, ambaye ni kizazi cha saba, cha wale walioishi Edeni, yeye alitembea na Mungu kwa karne tatu, asema, “Angalia Bwana alikuja na watakatifu wake, elfu, maelfu ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu. Kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake” Yuda 14:15. Ayubu naye katika usiku wa mateso alisema, “Najua ya kuwa Mtetezi wangu yu hai. Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi …. Nami nitamwona Mungu pasipokuwa na mwili wangu nitamwona, naam nafsi yangu mwenyewe. Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine” Ayubu 19:25-27. Mtunga zaburi na manabii wamenena juu ya kurudi kwa Kristo hivi: “Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie …. Mbele za Bwana, kwa maana anakuja, aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, na mataifa kwa uaminifu wake” Zaburi 96:11-13.TU 141.1

  Isaya naye asema, “Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie. Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake” Isaya 25:9.TU 141.2

  Mwokozi aliwafariji wanafunzi wake kwa uhakikisho wa kuja kwake, “Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi …. Nakwenda kuwaandalia makao …. Nikienda …. Nitakuja tena, niwakaribishe kwangu” “Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wake na malaika watakatifu wote pamoja naye. Ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake, na mataifa yote watakusanyika mbele zake” Yohana 14:2-3; Mathayo 25:31-32.TU 141.3

  Malaika walirudia kusema ahadi ya kurudi kwa Kristo wakisema, “Huyu atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni” Matendo 1:11 Paulo naye alishuhudia kwa kusema “kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu” 1Tes. 4:16. Nabii wa Patmo naye asema, “Tazama yuaja na mawingu na kila jicho litamwona” ufunuo 1:7.TU 141.4

  Halafu, ndipo uovu uliowatawala muda mrefu duniani utaangamizwa, “Falme za ulimwengu zimekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na Kristo wake, naye atamiliki milele na milele.” Ufunuo 11:15. “Bwana Mungu ataotesha haki na sifa mbele ya mataifa yote” Isaya 61:11.TU 141.5

  Ufalme wa Masihi ambao ni wa amani utasimamishwa. “Maana Bwana ataufariji Sayuni, atapafariji mahali pake palipokuwa ukiwa, atafanya jangwa lake kuwa kama bustani ya Edeni, nyika yake kama bustani ya Bwana”. Isaya 51:3.TU 142.1

  Kurudi kwake Bwana kumekuwa tumaini la wateule wake nyakati zote. Katika mateso na shida, kuonekana kwa mwokozi wetu na Mungu mkuu, kumekuwa tumaini lenye baraka. Tito 21:13. Paulo akitaja ufufuo utakaotokea wakati wa kuja kwa Bwana, wakati waliokufa katika Kristo watakapofufuliwa na walio hai kunyakuliwa pamoja ili kumlaki Bwana hewani, asema, “Hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele” “kwa hiyo farijianeni kwa maneno hayo”. 1 Thes. 4:17.TU 142.2

  Katika kisiwa cha Patmo mwanafunzi mpendwa alisikia ahadi ikisema, “Tazama naja upesi” jawabu lake ambalo ni maombi ya kanisa yasema, “amina, na uje Bwana”. Ufunuo 22:20. Tangu kule magerezani ambako watu wa Mungu walifungwa, na kwenye majiko walikochomea, na kule walikofia waaminifu wa Mungu, sauti zao za imani na tumaini hutujia katika karne zetu. Baada ya kuona hakika ya kuja kwake na ya ufufuo wa wafu, mkristo mmoja alisema, Walikidharau kifo, “wakakutwa wameshinda mauti” “Waldenses walishikilia imani hiyo. Wycliffe, Luther, Calvin, Knox, Ridley na Baxter, wote walikutazamia kurudi kwake Bwana katika imani thabiti. Hilo ndilo lilikuwa tumaini la kanisa la siku za mitume, na kanisa la Waldenses na tumaini la Watengenezaji kanisa (Reformers)”TU 142.3

  Unabii hauonyeshi jinsi na kusudi kwa kurudi kwa Kristo tu, lakini unaonyesha pia dalili za kuja kwake ambazo kwazo watu watafahamu wakati wa kuja.TU 142.4

  “Kutakuwa na ishara katika jua na mwezi na nyota”. Luka 21:25 “Jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota za mbinguni zitaanguka na nguvu za mbingu zitatikisika. Ndipo hapo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni na nguvu na utukufu mwingi.” Marko 13:24-26. Mwandishi wa ufunuo anaeleza hivi kuhusu dalili ya kwanza ya kurudi kwake Kristo. “Kulikuwa na tetemeko kuu, na jua likawa jeusi kama guni la singa, mwezi wote ukawa kama damu” Ufunuo 6:12TU 142.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents