Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jua Mwezi Kutiwa Giza

  Baada ya kupita miaka ishirini na mitano, ilionekana dalili nyingine tena iliyotajwa katika unabii, yaani jua kutiwa giza na mwezi pia. Muda wa kutukia dalili hizo ulitaja na mwokozi katika mazungumzo yake na wanafunzi wake. Alisema, “Lakini siku zile baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake” Marko 13:24. Miaka au siku 1260 ambazo ni za dhiki ile kuu zilimalizika mwaka 1798. Robo karne kabla ya muda huo haujamalizika, mateso yalikuwa karibu kukoma, ila kidogo tu. Kitakachofuata mateso hayo ni jua kutiwa giza. Tarehe 19 mei, 1780, dalili hii ilitimia.TU 143.3

  Mtu aliyeshuhudia tukio hilo huko Masachusetts alieleza hivi: “Wingu zito sana lilitanda mbinguni, likifunika mbingu nzima, ila nafasi ndogo pembeni, na ilikuwa giza kama inavyokuwa wakati wa kiangazi saa tatu za usiku….. Woga na wasiwasi viliwajaa watu. Wanawake walisimama milangoni mwa nyumba zao wakiangalia nchi katika giza. Wanaume waliokuwa wakifanya kazi katika mabanda ya ufundi walirudisha vyombo vyao. Shule zilifungwa na watoto wakarudi nyumbani katika hali ya hofu na kutetemeka. Wasafiri wakatua na kupiga kambi. Kitu gani kitatukia? Hilo ndilo lilikuwa swali la kila mtu. Ilionekana kwamba tufani kuu ilikuwa karibu kuvamia nchi, au jambo la uangamivu lingetokea na kuangamiza vitu vyote.”TU 144.1

  Mishumaa iliwashwa kana kwamba ni usiku wa giza pasipokuwa na mbalamwezi. Kuku waliingia kulala kama kawaida. Ng'ombe wakakusanywa na kulia, vyura wakalia, ndege wakaimba nyimbo za jioni, na popo wakaruka ruka kama wafanyavyo. Lakini watu walijua kuwa usiku bado haujaja.TU 144.2

  Watu walikusanyika mahali mahali. Mahubiri ya haraka haraka yasiyoandaliwa yakasomwa na kutaja mafungu yanayokubaliana na tukio hilo katika unabii. Giza lilizidi zaidi baada ya saa tano asubuhi.TU 144.3

  Mahali pengi nchini giza lilikuwa kubwa kiasi ambacho walishindwa kuona chochote bila mwanga wa mishumaa.TU 144.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents