Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Makundi Mawili Kanisani

  Kumekuwepo makundi mawili baina ya watu wajidaio kuwa wafuasi wa Kristo. Wakati kundi moja linajifunza maisha ya Kristo na linapojitahidi kufuata kielelezo chake kundi jingine linaepa kabisa kujifunza mambo ambayo yangedhihirisha makosa yao, maana hawataki kufuata ukweli. Walakini, hata kanisa lilipokuwa katika hali bora, halikuwa kamilifu kabisa. Yuda alihesabika kuwa mmojawapo wa wanafunzi ili kwa njia ya mafundisho ya Kristo na kielelezo chake angeweza kuona kasoro zake na kutubu. Lakini kwa ajili ya kushikamana na dhambi aliyakaribisha majaribu ya Shetani. Alichukizwa wakati kasoro zake zilipotajwa, na hivyo aliendelea mpaka akamsaliti Bwana wake. Marko. 14:10-11.TU 11.1

  Anania na Safira mkewe walijipendekeza kuwa wametoa mali yao yote kwa Mungu wakati walipoficha sehemu yake kwa choyo chao. Roho wa Mungu alimfunulia mtume Petro tabia yao hasa ya wajipendekezao hawa, na hukumu za usafi wa kanisa. Soma Matendo 5:1-11. Mateso yalipowajia wafuasi wa Kristo yaliwadhihirisha wale waliokuwa wafuasi halisi. Lakini mateso yalipokoma, wakaingia watu kanisani ambao hawakuwa wafuasi halisi, na kwa njia hiyo shetani alipata nafasi ya kuliharibu kanisa.TU 11.2

  Wakati wakristo waliporidhika kuungana na watu ambao hawakuongoka sawasawa, shetani alishangilia. Halafu aliwaamsha watu kama hao wawaudhi wale walioshikilia kanuni ya Mungu barabara. Wakristo wapotovu hawa ambao ni nusu wamizimu, walielekeza upinzani wao katika mafundisho yale ambayo ni muhimu kwa ukristo, ndiyo maagizo ya Kristo. Kutakikana msimamo imara kabisa kukabiliana na mafundisho mapotevu yaliyoingizwa kanisani. Biblia ilikataliwa wazi kuwa sicho kipimo cha ukristo. Uhuru wa dini ulihesabiwa kuwa kama uzushi na wale waliousikilia waliharamishwaTU 11.3

  Baada ya mapambano ya muda mrefu, wale waongofu wa kweli waliona kuwa ni lazima kuwepo utengano. Hawakuweza kuvumilia makosa hayo mabaya yenye kuleta hatari kwao na kwa watoto wao na wajukuu wao. Wakaona kuwa amani ya kweli lazima igharimu. Kwamba ikiwa kuwa na amani na kutupilia mbali kanuni za Mungu ndiko kutaleta umoja, basi amani ya namna hiyo na ipotelee mbali, ikilazimu lazima kuwe na utengano na hata kwa vita.TU 11.4

  Wakristo wa kwanza walikuwa waongofu wa kweli. Walikuwa wachache, bila kuwa na mali, heshima au vyeo nao walichukiwa na wale wamizimu, sawa kama vile Kaini alivyomchukia Habili. Soma Mwanzo 4:1-10. Tangu wakati wa Kristo mpaka leo, wafuasi wa kweli wa Mungu wamekuwa katika chuki na wale wapendao dhambi.TU 11.5

  Sasa basi, Injili itawezaje kuitwa kuwa ujumbe wa amani? Malaika waliimba katika uwanda wa Bethlehemu “Atukuzwe Mungu juu mbinguni na dunia iwe amani kwa watu aliowaridhia.” Luka 2:14. Inaonekana kuwa iko tofauti kati ya maneno haya ya Unabii na maneno ya Kristo: “Sikuja kuleta amani, bali upanga” Mathayo 10:34. Lakini yakifahamika kwa kweli, hayana tofauti yoyote. Injili na ujumbe wa amani. Dini ya Kristo ikipokelewa na kutiiwa hueneza furaha na amani duniani. Kazi ya Yesu ilikuwa kuwapatanisha watu na Mungu, mtu na mtu mwenzake. Lakini dunia kwa ujumla inatawaliwa na shetani, ambaye ni adui mkubwa wa Kristo. Injili inaonyesha kanuni za uzima na maisha kwa ujumla, na hizo hupingana na utawala wa shetani. Kanuni hizo za shetani hazitaki maisha matakatifu yanayokuwa kinyume na dhambi. Hilo huamsha vita kwa watu wanaong'ang'ania maisha matakatifu. Ni kwa njia hii ndiyo sababu Injili ikaitwa kuwa ni upanga. Soma Mat. 10:34.TU 12.1

  Watu wengi walio dhaifu katika imani wako tayari kuutupa ujasiri wao katika Mungu, kwa sababu huwafanikisha watu wabaya na watu wema husumbuka tu bila mafanikio. Mtu mwema, mwenye haki anawezaje kuchukuliana na hali ya jinsi hiyo isiyo na haki? Mungu ametuonyesha upendo wake kwa namna inayotosha. Hatuwezi kuona mashaka kwa wema wake, eti kwa sababu hatuelewi tu mipango yakeTU 12.2

  Mwokozi alisema: “Likumbukeni lile neno nililowaambia, mtumwa si mkuu kuliko Bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi” Yohana 15:20. Watu watakapopitia mateso, au hata mauti, huwa wamepitia njia ya Mwana mpendwa wa Mungu.TU 12.3

  Wenye haki hupitia katika mateso machungu ili watakase wao wenyewe, na njia hiyo iwe kielelezo cha imani yao kwa wengine na uongofu wa halisi ulivyo. Hali yao izibe vinywa vya wapotovu wanaosema kuwa haiwezekani kuwa hiyo. Mungu huwafanikisha waovu na kuudhihirisha uadui wao jinsi inavyowastahili adhabu ya uharibifu wao. Kila kitendo cha ufedhuli kitendewacho mtu wa Mungu, kitahesabika kana kwamba kilitendwa kwa Kristo mwenyewe, nacho kitaadhibiwa.TU 12.4

  Paulo asema, “Wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa” 2 Tim. 3:12. Kwa nini basi mateso yametulia? Sabatu yake ni kwamba kanisa limeungana na ulimwengu kimaisha, kwa hiyo hakuna upinzani wa kuchochea mashindano. Dini ya siku zetu hizi haifanani na ile ya siku za mitume katika utakatifu. Kwa kuwa ukweli wa Neno la Mungu unajaliwa kidogo tu, na kwa kuwa kuna uongofu kidogo tu kanisani, ukristo unakuwa kitu cha kawaida tu ulimwenguni. Hebu mwamko wa dini ya siku za mitume uwemo kanisani, hapo mto wa mateso utawashwa.TU 12.5

  Marejeo: TU 13.1

  Trertulian — Apology, paragraph 50TU 13.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents