Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwito Wa Kuamka

  Kuhusu siku hiyo kuu, neno la Mungu huwaita watu wake ili wautafute uso wake kwa njia ya toba hivi: “Kwa maana siku ya Bwana inakuja kwa sababu inakaribia”. “Takaseni sanamu, kusanyeni kusanyiko kuu. Kusanyeni watu, likataseni kusanyiko, kusanyeni wazee, kusanyeni watoto... Hao makuhani wahudumu wa Bwana, na walie kati ya patakatifu na madhabahu na waseme, Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga na kwa kulia, na kwa kuomboleza.” “Rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, makamrudie Bwana, Mungu wenu, kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema naye hughairi mabaya” Yoel 2:1, 15-17, 12-13.TU 146.1

  Kazi kuu ya matengenezo yaani kuwatayarisha watu ili kukutana na Mungu, budi ikamilishwe. Kwa rehema zake Mungu alikuwa tayari kuwatumia watu wake ujumbe wa Mungu alikuwa tayari kuwatumia watu wake ujumbe kuwaamsha ili wajitayarishe kwa kurudi kwake Yesu.TU 146.2

  Ujumbe huu umo katika Ufunuo 14; Hapa ndipo ujumbe wa sehemu tatu, unaowakilishwa kana kwamba ni tangazo linalotolewa na viumbe wa mbinguni warukao, ambalo hufuatiwa mara moja na kuja kwa Mwana wa Adamu ili avune mavuno ya nchi. Nabii aliona malaika akiruka katikati ya mbingu akiwa na Injili ya milele itakayohubiriwa kwa watu wote wakaao duniani, watu wa kila taifa na kabila na lugha na jamaa, ikisema kwa sauti kuu, “Mcheni Mungu na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake inakuja. Msujudieni yeye aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na chemichemi za maji.” Ufunuo 14:6-7.TU 146.3

  Ujumbe huu ni sehemu ya “Injili ya Milele”. Kazi ya kuhubiri ujumbe huu imekabidhiwa kwa wanadamu. Malaika watakatifu huongoza, walakini utangazaji hasa wa ujumbe ni wa watumishi wa Mungu waliomo duniani, watu waaaminifu, wanaofuata maongozi ya roho wa Mungu na kufuata mafundisho ya neno lake, ndiyo wanaohusika na utangazaji wa ujumbe huu. Wamekuwa wakitafuta maarifa ya Mungu, “wakiyahesabu kuwa ya thamani kuliko fedha na dhahabu. Siri ya Bwana iko kwao wamchao, naye atawaonyesha agano lake” Mithali 3:14; Zaburi 25:14.TU 146.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents