Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  18/Nuru Mpya Katika Ulimwengu Mpya.

  Mkulima mmoja mtawa, mwaminifu na mtafutaji wa ukweli, ndiye aliyeteuliwa na Mungu ili kukiongoza kikundi cha watu waliokutangaza kurudi kwake Yesu mara ya pili. William Miller aliishi maisha ya kimaskini, na ya kujikana kama watengenezaji wengine walivyoishi maisha ya kujinyima.TU 150.1

  Miller alijionyesha kuwa hodari na mwelekevu tangu utoto wake. Alivyoendelea kukua mawazo yake yalipanuka na kuendelea, naye alikuwa na kiu ya kupata elimu Upendo wake wa kujifunza, na nia yake thabiti, vilimsaidia kuwa mtu mwenye kufaa sana. Alikuwa na tabia njema na nyofu naye aliheshimiwa sana. Alijipatia cheo kikuu katika kazi zake za kiraia na za kijeshi pia. Kwa hiyo utajiri na heshima vilikuwa wazi kwake.TU 150.2

  Alipokuwa mtoto alivutiwa sana na mambo ya dini. Walakini alipokuwa mtu mzima alijikuta akiwa katika watu wanaoamini kuwa Mungu yuko aliyeumba vitu, lakini hana uwezo wa kuvitawala vitu hivo, ila kila kitu hujiendesha chenyewe kama kitakiwavyo. Watu hawa walimvutia sana, maana walikuwa watu wema, waungwana, wenye hali ya utawa. Miller alivutiwa na hali yao. Tabia yao iliwapatia sifa iliyotokana na Biblia, hata hivyo vipawa hivyo vyema viliharibiwa na kutoa mvuto wao katika Neno la Mungu.TU 150.3

  Sasa walivyoitafsiri Biblia kulileta tatizo kwake ambalo lilikuwa gumu sana. Lakini imani yake, isiyofuata kama Biblia inavyosema, haikumfaidia lolote, kama hakuridhika. Alipokuwa na umri wa miaka thelathini na minne roho Mtakatifu akimwangazia moyoni, akajiona kuwa yu mwenye dhambi. Hakuwa na uhakika wa maisha ya baadaye baada ya kufa. Kwa hiyo aliona giza tu kwa maisha ya mbele. Akajisemea moyoni hivi:TU 150.4

  “Mbingu ilikuwa ngumu juu ya kichwa changu, na nchi ilikwa kama chuma chini ya miguu yangu …. Kadiri nilivyofikiri, ndivyo mawazo yalivyotawanyika. Nilijaribu kujizuia nisiwaze, lakini sikuweza. Kwa kweli nilikata tamaa, kwa vile nilivyosindwa. Lakini sikuelewa sababu ya hali hiyo. Nililalamika na kugugumia, lakini kasoro gani, nami sikujua namna ya akuiondoa”.TU 150.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents