Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuja Kwa Kristo Waziwazi

  Mafundisho yasemayo kuwa ulimwengu mzima utaongoka, na kuwa ufalme wa kristo ni wa kiroho, hayakufundishwa na kanisa la mitume. Hayakukubaliwa na kanisa mpaka katika karne ya kumi na nane. Mafundisho hayo yaliwaelekeza watu kukutazamia kurudi kwa Kristo mbele sana, na ya kuwa dalili hizi zilizotajwa hazina maana. Kwa hiyo watu hawakujiandaa kwa kurudi kwake.TU 152.3

  Miller aligundua kuwa Kristo atakuja waziwazi, wala sio kiroho. Ndivyo Maandiko Matakatifu yasemavyo, “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu…” Nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni, pamoja na nguvu na utukufu mwingi ….. “Kwa maana kama hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu” …..“Atakapokuja mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake” 1Thes. 4:16-17; Mathayo 25:31; 24:31.TU 152.4

  Wakati wa kuja kwake watakatifu waliokufa watafufuliwa, na wenye haki walio hai watabadilishwa. “Hatutalala sote, lakini wote tutabadilishwa kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho, maana parapanda Italia na watu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, na sisi tutabadilika. Maana huu wa kuharibika sharti uvae kutokuharibika, na huu wa kufa sharti uvae kutokufa. Wafu katika Kristo watafufuliwa kwanza, kisha sisi tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao mawinguni ili kumlaki Bwana hewani, na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” 1Kor. 15:51-53; 1Thes. 4:16-17.TU 153.1

  Mtu katika hali aliyo nayo sasa, ni ya kufa na kuharibika. Kwa hiyo mtu katika hali aliyo nayo sasa hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu. Yesu ajapo ataondoa hali ya uharibifu kwa watu wake, kisha atawaita kuingia katika urithi wa ufalme wake, ambao wanakuwa warithi.TU 153.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents