Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Injili kwa Ulimwengu

  “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja” — Miaka saba ya mwisho wa wakati huo ilitolewa kwa ajili ya taifa la Wayahudi. Wakati huo wote, tangu 27 AD mpaka 34 AD Kristo na wanafunzi wake walieneza Injili kwa Wayahudi tu. Agizo la Kristo lilikuwa “Msiende kwenye njia ya mataifa, wala katika miji ya Samaria. Lakini nendeni kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli”. Mathayo 10:5-6.TU 156.1

  “Na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka ya dhabihu” Katika AD 31, miaka mitatu na nusu baada ya kubatizwa kwake, Bwana wetu alisulubishwa. Dhabihu kuu iliyotolewa huko Kalwari dhabihu za wanyama zilikoma. Huduma zote zilizokuwa kivuli zilikwisha.TU 156.2

  Miaka 490 iliyotolewa kwa ajilli ya Wayahudi ilimalizika katika A.D 34. Wakati huo kitendo cha bunge kuu la Kiyahudi cha kuamua kumwua Stefano kilifunga na kutiwa muhuri kanusho lao, kwamba hawana haja na Injili tena, nao wakaanza kuwatesa wafuasi wa Kristo na kuwaua. Hapo sasa Injili ya wokovu ikapelekwa kwa watu wa mataifa, katika ulimwengu wote. Wanafunzi waliolazimika kukimbia mateso kutoka Yerusalemu, “wakaendea huko na huko kila mahali wakilihubiri lile neno” matendo 8:4.TU 156.3

  Hivyo basi unabii ulitimizwa hatua kwa hatua kama ilivyopangwa. Mwanzo wa majuma sabini miaka 490 ni wa hakika hakuna shaka ni B.C 457, na mwisho wake ni A.D. 34. kwa kuwa majuma sabini yamekatwa katika 2300 kilichobaki ni miaka 1810. Baada ya kumalizika miaka 490 ile 1810 iliyobaki lazima nayo itimilike. Kutoka A.D. 34 miaka 1810 lazima iendelee mpaka 1844. Kwa hiyo siku au miaka 2300 ya unabii wa Danieli 8:14 zitakwisha katika 1844. Mwisho wa unabii huu mrefu, “ndipo patakatifu patakapotakasika”.TU 156.4

  Kwa hiyo wakati wa kutakaswa patakatifu unaaminia pote kuwa kutatokea wakati wa kurudi kwake Yesu.TU 156.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents