Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  “Nenda Uyatangaze Ulimwenguni”

  Asema, “Nilipokuwa nikifanya kazi, masikioni mwangu neno liliendelea kusikika likisema, ‘Nenda ukautangazie ulimwengu hatari inayoujilia’ Fungu hili lilinijia kila mara kusema: ‘Nimwambiapo mtu mwovu, Ee, mwovu, hakika utakufa katika uovu wako; kama wewe husemi na kumwonya mwovu huyo aache njia zake mbaya, hakika atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka katika mkono wako’ Niliona kuwa kama waovu wakionywa hakika, wengi wao watatubu; na kama hawakuonywa damu yao itadaiwa mkononi mwangu maneno haya yaliendelea kugoga katika dhamiri yake daima, yakisema, ‘Nenda, ukayatangaze ulimwenguni’ na damu yako nitaitaka mkononi mwako” Miller alingoja muda wa miaka tisa, huku mzigo wa nia hiyo ukizidi kumkandamiza, mpaka katika mwaka1831 ndipo kwa mara ya kwanza akajitokeza kueleza maana ya imani yake.TU 157.4

  Wakati huo alikuwa na umri wa miaka hamsini, ingawa hakuzoea kuhubiri mbele ya watu, lakini alifaulu. Hotuba yake ya kwanza iliwaamsha watu kidini. Familia kumi na tatu kasoro watu wawili, ziliongoka. Watu walichangamka sana kiroho, wakapata uvuvio mpya. Wakafiri na wenye mizaha wakauamini ukweli wa Biblia. Alihubiri huku na huko na kila mahali wenye dhambi walitubu. Mahubiri yake yaliwaamsha watu kiroho, na kukemea hali ya ulimwengu na ufedhuli vilivyokuwa vikihangaisha kizazi.TU 157.5

  Mahali pengi makanisa ya kiprotestanti ya madhehebu yote yalimsikiliza na kuamini, na miito ilikuja hasa kutoka kwa Wachungaji. Haikuwa kawaida yake kuhubiri mahali asipoitwa, hata hivyo miito ilikuwa mingi kiasi ambacho hakuweza kuitimiza yote. Watu wengi walithibitika na kuamini kuwa Kristo yu karibu kurudi, na haja yao kujiweka tayari. Katika miji mingi wenye maduka ya kuuza vileo waliyageuza maduka yao kuwa sebule za mikutano ya dini. Wacheza kamari waliacha; makafiri na wafedhuli mno waligeuka, kila mtu akafanya matengenezo ya dini. Mikutano ya ibada ilifanyika, na kuendeshwa karibu kila saa na madhehebu yote, hata wenye biashara walikuwa wakikutana kwa ibada na maombi. Hapakuwapo na msisimko wa ovyo ovyo. Kazi yake ilifanana na ile ya watengenezaji, yaani kuwafikisha watu wala sio kuwasisimua tu.TU 158.1

  Katika mwaka 1833 Miller alipata hati ya kuhubiri kutoka katika kanisa la Baptist. Wachungaji wengi wa kanisa walikubaliana na mafundisho yake. Alisafiri akihubiri bila kukoma na wala hakuwa na fedha za kutosha kujibu miito yote. Kazi hiyo ilimgharimia fedha nyingi zake binafsi.TU 158.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents