Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Nyota Zaanguka

  Katika mwaka 1833 dalili ya mwisho iliyosemwa na Mwokozi kuwa ni ishara ya kuja kwake, ilionekana. “Nyota zitaanguka kutoka mbinguni”. Na Yohana katika ufunuo husema, “Na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi”. Mathayo 24:29; ufunuo 6:13.TU 158.3

  Unabii huu ulitimizwa kabisa katika maanguko ya nyota ya November 13, 1833, ambayo ni ya ajabu kabisa yasiyopata kutokea kabla ya hapo. Mvua haijanyesha kamwe kwa wingi nchni kama zilivyoanguka nyota hizo. Pande zote, mashariki, magharibi, kaskazini na kusini hali ilikuwa ile ile. Kwa kifupi ni kwamba mbingu ilionekana kana kwamba inatikisika ….. Tangu saa mbili asubuhi mpaka mchana mmemetuko na yota zilivyokuwa zikianguka.TU 158.4

  Ilionekana kana kwamba nyota zimekusanyika mahali pamoja, na sasa zinaanguka kwa kumetameta kwa mng'aro mkubwa, kutoka pande zote. Zilionekana kufuatana kwa maelfu kwa mfano wa mitini upukutishavyo mapoozo yake.TU 159.1

  Katika gazeti la New York ilionekana habari ndefu iliyoandikwa kuhusu tikio hilo, ikisema, “Hakuna mtaalamu yoyote aliyeweza kuandika usahihi wa tukio hilo. Nabii aliyetabiri tukio hilo miaka 1800 iliyopita ndiye alisema kwa usahihi anguko la nyota. Hivyo ndivyo dalili ya mwisho ya kuja kwa Kristo ilivyotokea, ambaye Yesu aliwaambia wanafunzi wake akisema ‘Ninyi myaonapo hayo yote, fahamuni kuwa yu karibu tena milangoni’ Mathayo 24:33. Wengi walioshuhudia kuanguka kwa nyota walikuhesabu kuwa tangazo la kuja kwa hukumu ya Mungu.”TU 159.2

  Katika mwaka 1840 jambo jingine la unabii lilitukia likishangaza watu. Miaka miwili kabla, Josia Litch alitangaza, na kueleza habari ya ufunuo 9 ikitabiri anguko la dola ya Ottoman katika mwaka 1840, katika mwezi wa Agosti. Aliandika siku chache mbele akisema, “Itaanguka katika Agost 11, 1840, wakati uwezo wa Ottoman utakapoangamia katika Constantinople”TU 159.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents