Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wakaidi na Wasioamini

  Kristo alisema kuwa jinsi watu wa siku za Nuhu “wasitambue, hata gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu”. Mathayo 24:39. Wakati watu wa Mungu watakapounganika na ulimwengu, wakati anasa za dunia zitakapoingia kanisani, wakati wote watakapotazamia siku 7 za mafanikio duniani, ndipo kwa ghafla, kama umeme umulikavyo, ndivyo utakavyokuwa mwisho wa matumaini yao. Jinsi Mungu alivyomtuma mtumishi wake kuwaonya walimwengu wa siku za Nuhu juu ya gharika, ndivyo atakavyowatuma watumishi wake waaminifu kutangaza ukaribu wa kuja hukumu yake, na jinsi watu wa Nuhu walivyomcheka na habari aliyotangaza, kadhalika siku za Miller watu walidhihaki maonyo yake.TU 161.4

  Hakuna ushahidi zaidi kuliko huu ya kwamba makanisa yaliyojitenga na Mungu yanaudhihaki ujumbe uliotumwa na Mungu.TU 161.5

  Wale walioupokea ujumbe wa marejeo waliona kuwa huu ndio wakati wao wa kuwa na msimamo halisi. Mambo ya milele yameingia katika nia zao hakika. Mbingu ilikaribiana nao, nao wakajiona kuwa ni wenye hatia mbele za Mungu Wakristo walijisikia kuwa wakati walio nao ni mfupi sana, na kwamba yawapasayo kuwafanyia wenzao, budi yafanye upesi. Umilele ulionekana kufika karibu. Roho wa Mungu aliwawezesha kujitayarisha kwa ajili ya siku ya Mungu. Maisha yao ya unyofu yaliwahukumu wasiomcha Mungu, ambao ni wakanisa, maana hawakutaka kuingiliwa katika shughuli zao za anasa na uchumi, na upendo wa ulimwengu. Hayo yote yalileta upinzani kwa watu wa marejeo.TU 161.6

  Wapinzani hawa walijitahidi kuwakatisha tamaa, kwamba unabii wa hukumu ya Mungu umefungwa, hauna haya kushughulikiwa. Na kwa jinsi hii Waporotestanti walifuata njia ya Rumi. Waprotestanti walidai kwamba jambo la muhimu linalohusu wakati wetu haliwezi kufahamika, maana limefungwa. Wahubiri wakasema kuwa vitabu vya Danieli na ufunuo ni vya siri zisizojulikana.TU 162.1

  Lakini Kristo aliwaelekeza wanafunzi wake katika maneno ya Danieli kuwa, “Asomaye na afahamu” Mathayo 24:15 na Ufunuo pia utafahamika. “Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwa upesi. Heri asomaye, na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu” ufunuo 1:1-3.TU 162.2

  “Heri asomaye” - kutakuwa na watu wasiosoma. “Na wale wao wayasikiao” — Kuna watu wanaokataa kusikiliza kitu chochote cha unabii. “Na kuyashika yalioandikwa humo” - Wengi hukataa kushika mafundisho ya ufunuo. Hawa hawana udhuru, wala hawatapata mibaraka iliyoahidiwa.TU 162.3

  Watu wanathubutuje kusema kuwa ufunuo hautafahamika? Ni siri iliyofunuliwa, kitabu kilicho wazi. Ufunuo huongoza mawazo kuelekea Danieli. Vitabu vyote hutoa mafundisho yahusuyo matukio ya siku za mwisho.TU 162.4

  Yohana aliona hatari, mapambano, na mwisho aliona ukombozi wa watu wa Mungu. Aliandika juu ya ujumbe wa mwisho utakaoyakomaza mavuno ya nchi, yaani wafuasi wa Mungu. Mavuno ya aina mbili, yale yatakayopelekwa mbinguni na yale yatakayochomwa motoni. Kwa hiyo wale wanaogeuka kutoka katika ukafiri na kuingia katika nuru, hupata mafundisho ya siku za mwisho kuhusu hatari na mapambano yanayowakabili.TU 162.5

  Kwa nini basi watu huishi ujingani kuhusu mafundisho ya Danieli na Ufunuo, ambayo ni sehemu ya maandiko Matakatifu? Ni makusudi ya yule mwovu kuwafunga watu wadumu gizani wasiyajue mambo yajayo yanayofunua udanganyifu wake. Kwa ajili hii Kristo mfunuaji wa siri, aliona jinsi vitabu hivyo vitakavyopigwa vita, ndipo akasema, “Heri asomaye” naye “Asikiaye”. Na “Kuyashika”, mambo ya unabii huu.TU 163.1

  Marejeo: TU 163.2

  S. Bliss Memories of William Miller, pp. 65-67 TU 163.3

  Ibidi., pp. 74-75 TU 163.4

  Ibid., 76-77, 81 TU 163.5

  Ezekiel 33:8-9 Bliss, p. 92 R.M Devens. American Progress of The Great Events of Greatest Century, ch. 28 para. 1-5 TU 163.6

  F. Reed — Christian Advocate and Jounal, Dec. 13, 1833 TU 163.7

  The Old Countryman — Portland (Maine) TU 163.8

  Evening Advertiser, Nov. 26, 1833 TU 163.9

  Josiah Litch — Signs of the Times, August 1, 1840 TU 163.10

  Bliss, pp. 250, 252 TU 163.11

  Ibid., p. 146TU 163.12

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents