Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  19/Kwa Nini Uchungu Mkuu?

  Kazi ya Mungu hufanana sana kizazi hata kizazi na karne hadi karne, wakati matengenezo makuu ya uamsho yanapofanyika. Kanuni za Mungu za kuongezea watu ni zile zile. Msimamo wa kanisa kwa wakati huu ni sawa na wa wakati uliopita, na msimamo wa kanisa wa wakati uliopita unalo fundisho kwa wakati huu.TU 164.1

  Mungu huwaongoza watumishi wake kwa njia ya Roho wake ili kuendesha kazi yake duniani. Watu huwa vyombo tu katika mkono wake. Kila mtu amepewa nuru ya kutosha kufanyia kazi aliyokabidhiwa. Lakini hakuna hata mtu ye yote aliyepata kufahamu mambo yote ya Mungu kwa wakati wake. Watu hawaelewi mambo yote yapasayo kazi ya Mungu wanayofanya. Hata manabii hawakufahamu ujumbe wote na mafunuo waliyofunuliwa. Maana ya maono hayo ilikuwa ikifunuliwa taratibu karne kwa karne.TU 164.2

  Petrol asema, “Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta tafutta na kuchunguza chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulionywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakao kuwako baada ya hayo. Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu.” 1 Petro 1:10 - 12. Katika kizazi cha ukristo, hilo ni fundisho muhimu kiasi gani! Wale watu watakatifu wa Mungu walitafutatafuta kwa bidii, mambo yaliyofunuliwa wakati wa vizazi ambavyo havijazaliwa bado. Jambo hili linakanusha usemi wa wakristo wanaostarehe tu na kusema kuwa unabii haufahamiki.TU 164.3

  Sio kwa nadra akili hata za watumishi wa Mungu huwa vipofu wakabaki kufuata mapokeo tu na hadithi za mafundisho ya uongo, kwamba hushika mambo yaliyofunuliwa katika Neno la Mungu sehemu sehemu basi. Wanafunzi wa Kristo, hata wakati ule Mwokozi alipokuwa pamoja nao walikuwa na mawazo hafifu kuhusu Masihi, kwamba ni mtawala wa muda tu atakayekuja kuwasaidia. Wala hawakuyafahamu maneno yake kuhusu mateso yake na kifo chake.TU 164.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents