Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wakati Umetimia

  Kristo aliwatuma wakiwa na ujumbe wake kwamba: “Wakati umetimia”, na “ufalme wa Mungu umekaribia: tubuni mkaiamini Injili.” Marko:15. Unabii huo ulikuwa umejengwa katika Danieli 9. Majuma sitini na tisa yataendelea mpaka kwa Masihi Mkuu. Wanafunzi walitazamia kwamba masihi atausimamisha ufalme katika Yerusalemu, ili kuitawala nchi yote.TU 165.1

  Walihubiri ujumbe waliokabidhiwa, ingawa walikosa kuielewa maana yake halisi. Ijapokuwa mahubiri yao yalisimama katika Danieli 9:25 hawakuliona fungu lililofuata lisemalo kwamba Masihi atakatiliwa mbali. Mawazo yao yalikuwa tu juu ya utukufu wa ufalme utakaosimamishwa duniani. Hili liliwapofusha kabisa. Wakati ule walipotazamia Bwana wao kuwa mfalme katika kiti cha Daudi, walimwona akikamatwa, na kuteswa, na kudhihakiwa na mwisho kufa msalabani. Kwa hiyo walivunjika na kukata tamaa kiasi gani!TU 165.2

  Kristo amekuja katika wakati ule ule ilivyotabiriwa. Maandiko yametimizwa kwa ukamilifu kabisa. Neno la Mungu na Roho wa Mungu wameshuhudia agizo la mbinguni kuhusu Mwana wa Mungu. Walakini mawazo ya wanafunzi yalikuwa yamejazwa na mashaka tu. Je, kama Yesu angekuwa Masihi kweli wangejazwa na masikitiko, na uchungu? Hilo ndilo swali lililokuwa likiwahangaisha siku hiyo ya Sabato baina ya kifo chake na kufufuka kwake.TU 165.3

  Hata hivyo hawakukataliwa na kuachwa, “Nikaapo gizani Bwana atakuwa nuru kwangu..... atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake.” “Nuru huwa-zukia wenye adili gizani.” “Nitafanya giza kuwa nuru mbele yao, na mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya nitayatenda, wala sitawaacha.” Mika 7:8,9; Zaburi 112:4; Isaya 42:16.TU 165.4

  Matengenezo yaliyotangazwa na wanafunzi yalikuwa sawa, kwamba, “Wakati umetimia, ufalme wa Mungu umekaribia.” Mwisho wa wakati ule, - yaani majuma sitini na tisa ya Danieli 9, ambayo yangeeendelea mpaka Masihi, mwenye kutiwa mafuta, ndiye Kristo aliyetiwa mafuta ya Roho Mtakatifu alipobatizwa na Yohana Mbatizaji. Ufalme wa dunia haukuwa ufalme wa wakati huo wa milele ambao falme zote zitamtumikia. Danieli 9:27.TU 165.5

  Neno, “ufalme wa Mungu,” humaanisha ufalme wa neema na ufalme wa utukufu. Mtume husema, “Basi na tukaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema wakati wa mahitaji.” Waebrania 4:16. Kuwapo kiti nikuwapo ufalme. Kristo hutumia neno, ufalme wa mbinguni, kumaanisha kazi ya neema mioyoni mwa wanadamu. Kwa hiyo kiti cha utukufu humaanisha ufalme wa utukufu. Mathayo 25:31, 32. Ufalme huu ni wa baadaye, utasimamishwa katika kurudi kwake Yesu.TU 165.6

  Wakati Mwokozi alipotoa maisha yake na kulia, “Imekwisha”, ahadi iliyotolewa kwa Adamu na Hawa huko Edeni ilithibitishwa. Ufalme wa neema ambao kwanza ulikuwako kwa njia ya ahadi tu, ukasimikwa.TU 166.1

  Hivyo basi kifo cha Kristo, tukio ambalo wanafunzi walidhani kuwa limeharibu tumaini lao, ndicho kilithibitisha uhakika wa tumaini lao milele. Ingawa kilikuwa na ukatili wa hali ya juu kabisa, ndicho kilihakikisha kuwa imani yao ni ya hakika. Tukio lililowatia uchungu na kukata tamaa, lilifungua mlango wa tumaini kwa watu wa Mungu wa nyakati zote. Kwa kuchangamanisha upendo halisi kwa Yesu na anasa ndiko kuliwafanya wanafunzi wakakuza ubinafsi wa tamaa ya kutaka vyeo. Njozi zao zilijazwa na enzi na taji za kifalme na utukufu wake, kiburi chao, kiu yao ya heshima viliwaongoza, nao hawakuyajali mafundisho ya Kristo yahusuyo ufalme wa neema, na yale yahusuyo mauti yake. Makosa haya yalileta matokeo ya majaribu yaliyowapata ili kuwarekebisha. Kwao Injili ya utukufu itakayotangazwa ulimwenguni, ilikabidhiwa. Injili hiyo ni ya kufufuka kwake Mwokozi. Ili kuwaandaa kwa kazi hiyo, majaribu makali yaliwapitia.TU 166.2

  Baada ya kufufuka kwake Yesu, aliwatokea wanafunzi wake waliokuwa wakienda Emau, na kuwafunuliwa mambo yote yaliyomhusu yeye, kama Maandiko yasemavyo. Lilikuwa kusudi lake kukaza imani yao juu ya unabii (Luka 24:27; 2 Petro 1:19) si kwa kumwona yeye binafsi, ila kufuata unabii wa agano la Kale. Kama hatua ya kwanza ya kuwafundisha, Yesu alielekeza mawazo yao juu ya Musa na manabii wote wa agano la Kale.TU 166.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents