Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kufa Moyo Hadi Ushindi

  Sasa wanafunzi walimpata kwa hakika yule ambaye Musa na manabii waliandika habari zake. Sasa mashaka na kukata tamaa vimetoweka, na badala yake wamekuwa na imani na ushindi kamili. Wamepita katika kipindi kigumu, na mwisho wameona jinsi neno la Mungu lilivyoshinda na kutimia. Sasa ni nini tena kitawatatanisha? Katika masikitiko makuu wamepata ushindi na tumaini la hakika, ambalo ni sawa sawa na nanga iliyo imara. Waebrania 6:18, 19.TU 166.4

  Bwana asema, “Watu wangu hawataaibika milele”, “Huenda kilio huja kukaa usiku, lakini asubuhi huwa furaha.” Yoeli 2:26; Zaburi 30:5. Siku ya kufufuka kwake Bwana wanafunzi hawa walimlaki, na roho zao ziliburudika wakati walipokuwa wakisikiliza maneno yake. Kabla ya kupaa kwake kwenda mbinguni, Yesu aliwaagiza wanafunzi, akisema, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili.” Akaongeza kusema, “tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote.” Marko 16:15; Mathayo 28:20. Siku ya Pentekoste Mfariji aliyeahidiwa alishuka, na roho za wanafunzi zikaburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.TU 167.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents