Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ujumbe wa wanafunzi Ulifanana na wa 1844

  Hali ya mambo ilivyokuwa wakati wa mwanzo wa marejeo ya Kristo, ndivyo pia ilivyokuwa kwa wale waliokutangaza kurudi kwake mara ya pili. Jinsi wanafunzi walivyohubiri kwamba, “Wakati umetimia, ufalme wa mbinguni umekaribia”, ndivyo hivyo Miller pia na wenzake walivyohubiri kwa kipindi cha unabii cha mwisho katika Biblia kilikuwa karibu kumalizika, na kwamba hukumu iko karibu, na ufalme wa milele uko karibu. Mahubiri ya wanafunzi kuhusu wakati yalijengwa juu ya Danieli 9. Ujumbe uliotangazwa na Miller na wenzake ulikuwa ukisema kuwa unabii wa siku 2300 ulikuwa karibu kumalizika, Unabii huo umo katika Danieli 8:14, ambao sehemu yake ni majuma sabini. Mahubiri yote hayo yalihusu utimizo wa nyakati tofauti katika unabii ule ule wa muda ule ule.TU 167.2

  Sawa na wale wanafunzi walivyokuwwa, hali kadhalika William Miller na wenzake hawakuelewa kamili ujumbe waliokuwa wakiuhubiri. Makosa ambayo yalikuwa kanisani yaliwazuia wasiutafsiri vizuri unabii. Kwa hiyo ingawa walikuwa wakihubiri ujumbe wa Mungu, lakini kwa kukosa kuutafsiri vizuri, waliangukia katika hali ya uchungu na kukata tamaa.TU 167.3

  Miller alishikilia maoni ya wengi kwamba nchi hii ndiyo “patakatifu”, na akaamini kuwa kutakaswa kwa patakatifu ni kule kuchomwa moto wa utakaso wa dunia. Moto huo ni ule wa wakati wa kuja kwa Bwana, yaani mwisho wa dunia. Kwa hiyo akaamua kuwa mwisho wa siku 2300 ni wakati wakuja kwa Bwana mara ya pili.TU 167.4

  Utakaso wa patakatifu kilikuwa kitendo cha huduma ya mwisho ya kuhani mkuu, kwa kila mwaka. Ilikuwa huduma ya upatanisho inayofunga huduma zote katika mwaka mzima, yaani kuondoa dhambi zote katika Israeli. Ilikuwa ni kivuli cha huduma ya Kuhani wetu Mkuu huko mbinguni, yaani huduma ya kuondoa dhambi za watu wake zilizoandikwa vitubuni mbinguni. Kazi hii inahusu upelelezi au uchunguzi na hukumu, ambayo inatangulia kuja kwa Bwana mbinguni. Wakati Bwana akija kila jambo litakuwa limeamuriwa. Yesu asema, “Na ujira wangu u pamoja nami kumlipa kila mtu kwa kadiri ya kazi, au matendo yake.” Ufunuo 22:12. Kazi hii ndiyo iliyotangazwa katika ujumbe wa malaika wa kwanza wa Ufunuo 14:7, kwamba, “Mcheni Mungu na kumtukuza, maana saa ya hukumu yake imekuja.”TU 168.1

  Watu wanaoutangaza ujumbe huu, hutangaza ujumbe wa kweli, na wakati ufaao. Jinsi wanafunzi walivyokosea kuhusu ufalme utakaosimamishwa mwisho wa “majuma sabini”, hali kadhalika watu wa Marejeo walikosa kuhusu tukio litakalotukia mwisho wa siku 2300. Katika mambo yote mawili maoni ya watu yaliwapoteza. Wote walitimiza mapenzi ya Mungu kwa kutangaza ujumbe, ambao ulipaswa utolewe na wote wakaangukia katika masikitiko na uchungu mkali, kwa ajili ya kutafsiri vibaya unabii.TU 168.2

  Walakini Mungu alitimiza kusudi lake la kutangaza kwa ujumbe wa hukumu kama ilivyokusudiwa. Kwa maandalio yake, ujumbe ulileta jaribu na utakaso wa kanisa. Je, nia zao zilikazwa ulimwenguni au mbinguni? Je, walikuwa tayari kuukana ulimwengu na kumlaki Bwana? Ule msiba wa uchungu ungewapima watu wanaojidai kuwa wafuasi wa Mungu, kama watayapokea maonyo. Je wangekuwa tayari kumtegemea Mungu kamili wakati walimwengu wanapowazomea? Wangevumilia uchungu wa kutokurudi Bwana wao? Kwa kuwa hawakufahamu jinsi Mungu anavyofanya, Je, wangeutupilia mbali ule ukweli unaothibitika katika neno lake?TU 168.3

  Jaribu hili litatoa fundisho kuhusu kukubaliana na tafsiri za binadamu, badala ya Neno la Mungu hasa. Wana imani watajitahidi kuchunguza Biblia, ili kupima msimamo wao na kukataa kitu chochote ingawa kinakubaliwa na wakristo ulimwenguni, kitu ambacho hakipatikani katika Maandiko Matakatifu.TU 168.4

  Mambo ambayo wakati wa majaribu huonekana kuwa giza, baadaye yatakuwa dhahiri. Ingawa majaribu yatokane na makosa yao, lakini kwa maongozi ya Bwana, ambaye “Njia zote za Bwana ni fadhili na kweli, Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.” Zaburi 25:10.TU 169.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents