Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  3/Giza la Kiroho Katika Kanisa la Kwanza

  Mtume Paulo aeleza kwamba siku ya Kristo haitakuja “Usipokuja kwanza ule ukengeufu, akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu. Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi”. 2Wathesalonike 2:3,4-7. Hivyo hata siku hizo za mwanzoni mtume aliona uovu ukilitambalia kanisa ambao utaingiza upapa ndani.TU 14.1

  Kidogo kidogo, “siri ya kuasi” iliendesha kazi yake ya udanganyifu. Kawaida za kimizimu ziliingizwa kanisani na kukubaliwa kuwa nia sawa, ingawa zilipingwa kwanza na kuleta mateso kwa njia ya wamizimu. Lakini mateso yalipokoma hali ya kanisa ilibadilika na kuacha kanuni halisi ya kikristo. Hali hiyo iliongozwa na mapapa na mapadri. Uongofu bandia wa mfalme Constatine ulileta burudiko kubwa kanisani. Kwa hiyo sasa uharibifu ulizidi mno kanisani. Ukafiri ulishinda kabisa na kutawala kanisani. Kawaida za kikafiri na mafundisho ya ushirikina viliingizwa kanisani na kuhesabiwa kuwa ni mojawapo ya kanuni za Kikristo.TU 14.2

  Mapatano haya baina ya ukafiri na ukristo yalitokeza “mtu wa dhambi”, aliyetabiriwa katika Biblia. Dini ya uongo ni hila za Shetani, na juhudi yake ni kuketi katika kiti cha enzi apate kuutawala ulimwengu kama apendavyo.TU 14.3

  Mojawapo ya mafundisho ya kanisa la Kiroma ni kwamba papa amepewa uwezo mkuu awe juu ya makasisi wote na wachungaji wote wa ulimwengu. Zaidi ya hayo, papa amepewa heshima ya kuitwa “Bwana Mungu Papa” na kwamba yeye hakosei hata kidogo. Dai lile lililodaiwa na shetani huko jangwani wakati wa majaribu ya Yesu lingali linaendelea katika kanisa la Kirumi; na watu wengi humtukuza jinsi hiyo.TU 14.4

  Lakini wanaomcha Mungu huyapinga majivuno hayo kama Kristo alivyoyapinga ya mwovu shetani jangwani. “Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake” Luka 4:8. Kamwe Mungu hakumweka mtu ye yote kuwa kichwa cha kanisa. Ukuu wa upapa unapingwa na Maandiko Matakatifu. Papa hawezi kuwa kichwa cha kanisa la Kristo isipokuwa ajitwalie mamlaka hayo kwa nguvu. Warumi hawalaumu waprotestanti, na kusema kwamba wamejitenga na kanisa la kweli. Lakini wao ndio waliojitenga na Imani “ambayo kwanza ilikabidhiwa kwa watakatifu” Yuda 3.TU 14.5

  Shetani alifahamu fika kuwa Mwokozi aliyapinga majaribu yake kwa njia ya Maandiko Matakatifu. Kila jaribu la shetani Mwokozi alilipinga kwa ngao ya kweli, akisema “Imeandikwa”. Ili kusudi shetani awashinde watu, na wasifahamu Maandiko Mataktifu. Ukweli Mtakatifu lazima ufichwe usifahamike. Kwa muda wa miaka mamia Biblia ilikatazwa kusomwa kabisa na kanisa la Kirumi. Watu waliruhusiwa kusoma na kueleza maana yake, ili kufaulisha mpango wao. Kwa njia hiyo Papa alitukuzwa kabisa ulimwenguni kama kaimu wa Mungu duniani.TU 15.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents