Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uwezo Kitabuni

  Dr. Wolff alisafiri katika nchi nyingi za watu wakorofi bila kuwa na ulinzi wo wote, huku akivumilia shida nyingi sana, na kupita katika hatari za kila namna. Alikuwa akishinda njaa; akiuzwa kama mtumwa, mara tatu alihukumiwa kufa, akishambuliwa na wanyang'anyi, na mara nyingine akiwa karibu kufa kwa kiu. Mara moja alitekwa na kutembezwa maili mamia kwa miguu, akipitishwa milimani kwenye barafu akiwa karibu uchi.TU 172.4

  Alipoonywa kuwa asitembee katikati nchi za makatili bila kuwa na ulinzi kamili, alisema kuwa yeye anazo silaha kamili, ndiyo maombi na matumaini yake kwa Kristo. Silaha nyingine niliyo nayo ni upendo wa Mungu nilio nao moyoni mwangu anaoniwezesha kuwapenda watu wengine. Na Biblia niliyo nayo mkononi mwangu ndiyo silaha mahsusi. Kitabu hiki cha Biblia ndiyo nguvu yangu. Ndicho msaada wangu.TU 173.1

  Aliendelea hivyo mpaka sehemu kubwa ya nchi ikasikia ujumbe. Alieneza Injili na kutoa sehemu za Injili kwa baadhi ya Wayahudi, Waturuki, Waparisi, Wahindu na mataifa mengineyo. Kila mahali alikutangaza kurudi kwa Masihi kuliko karibu sana.TU 173.2

  Katikati ya Bokhara alikuta kikundi cha watu wakikutangaza kurudi kwake Bwana. Alisema, Waarabu wa Yemen wanacho kitabu cha Seera, ambacho hueleza habari za kurudi kwake Bwana, na kumiliki kwake kwa fahari watu hao anakutazamia kurudi kwa Bwana kutatokea katika mwaka 1840 ….. Niliwakuta wana wa Israeli wa kabila la Dani pamoja na wana wa Rekabu wakikutazamia kurudi kwa Bwana kwa hamu sana.TU 173.3

  Imani hiyo hiyo ilionekana katika Wamishenari wengine wa Tatari. Kuhani wa Tatari aliuliza kuwa, ni lini Kristo atarudi pamoja na mawingu? Huyo mtu wa misheni alipoonekana kuwa hana habari, yule Kuhani wa Tatari alishangaa sana kuwa mwalimu huyu wa Biblia hana habari juu ya jambo hili. Huyu mtu wa Tatari alionyesha imani yake kwa yale yaliyomo katika unabii kwamba Kristo atarudi katika mwaka wa 1844.TU 173.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents