Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ujumbe wa Marejeo Huko Uingereza

  Ujumbe wa marejeo ulihubiriwa Uingereza mapema kama mwaka 1826. Ujumbe kamili haukuhubiriwa, lakini habari ya kurudi kwake Kristo katika mawingu ilikuwa imetangazwa. Mwandishi mmoja aliandika kwamba, kiasi cha Wachungaji 700 wa kanisa la Anglikana (uingereza) walikuwa wakihubiri kuhusu “Injili hii ya” “Ufalme”TU 173.5

  Injili iliyokuwa ikitaja kuwa Kristo atarudi mwaka 1844 ilikuwa ikihubiriwa huko Uingereza. Magazeti yaliyohusu marejeo ya Kristo yalichapishwa Marekani yalikuwa yakitolewa kwa wingi huko Uingereza. Katika mwaka 1842 Robert Winter, mwingereza aliyeukubali ujumbe wa marejeo huko Marekani, alirudi nyumbani kwao kutangaza ujumbe huo. Watu wengi walijiunga pamoja naye katika kazi hiyo ya kutangaza, katika sehemu kadhaa za Uingereza.TU 174.1

  Huko Amerika ya Kusini Lacunza, mtu wa Hispania wa dhehebu la Jesuit, aliupokea ujumbe wa marejeo akauamini. Ili kusudi kuepuka maalumu ya Rumi, aliandika habari zake, akijiita kuwa Mwalimu Ben-Ezra, akijipendekeza kuwa ni mwongofu wa Kiyahudi. Panapo mwaka 1825 kitabu chake kilitafsiriwa katika lugha ya kiingereza. Kitabu hicho kiliongezea mkazo wa imani juu ya ujumbe ambao umeshahubiriwa tayari, huko Uingereza.TU 174.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents