Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Aliyofunuliwa Bengel

  Katika Ujerumani mafundisho ya Biblia yalikuwa yamefundishwa na Bengel, mchugnaji wa Kiluther. Alipokuwa anatayarisha mahubiri kutoka katika ufunuo 21 nuru ilimulika katika mawazo yake kuhusu kurudi kwa Yesu. Ufunuo wa unabii uling'aa mawazoni mwake na akashangaa kwa fahari ya kurudi kwake Kristo, kama ilivyoelezwa na nabii. Alitafakari kwa muda habari hiyo. Hata alipokuwa mimbarani, fahari ya kurudi kwake Yesu iling'aa tena mawazoni mwake. Tangu wakati huo alijitia katika kujifunza habari za unabii, na halafu ukafikia uamuzi kuwa Kristo atakuja upesi. Muda aliodhani kuwa Yesu atarudi ulikuwa karibu na ule wa Miller.TU 174.3

  Maandiko ya Bengel yalienezwa kwanza katika mkoa wa kwao wa Wirtemberg, na baadaye yakaendea katika nchi nzima ya Ujerumani, na wakati huo kuvutia na nchi nyingine pia.TU 174.4

  Huko Geneva Gaussen alihubiri kuhusu kurudi kwake Kristo. Alipoingia katika kazi ya kuhubiri alielekea kuwa mtu wa mashaka. Wakati wa ujana wake alikuwa anapenda sana mambo ya unabii. Baada ya kusoma kitabu cha Rollins, juu ya “Historia ya Kale”, ilielekezwa mawazoni juu ya Daniel sura mbili. Alishangazwa na jinsi unabii ulivyotimia bila kukosa, hata kidogo. Huu ulikuwa uthibitisho wa uvuvio wa Maandiko Matakatifu. Basi hakutosheka na imani ya juu juu. Alipoendelea kuchunguza Biblia zaidi, alibadili imani yake ya kwanza.TU 174.5

  Alifikia uamuzi ya kwamba kurudi kwa Yesu kuko karibu. Alipokuwa na imani hiyo, alitamani kuwafunulia na watu wengine pia. Lakini watu waliokuwa hawauamini unabii wa Daniel walimpinga vibaya. Mwisho akaazimu kufundisha watoto, sawa kama Farel alivyofanya Geneva. Alitumaini kuwa watoto wakiamini watawavuta wazazi wao. Alisema, “Nilikusanya kundi la watoto, kama watoto hawa watasikiliza, nina hakika kuwa nitapata kundi la pili; na kwa hiyo hata wazazi wataingia”. Jambo hili likifanyika, kazi imetimilika.TU 175.1

  Alipofundisha watoto, watu wazima pia walikuja kusikiliza. Basi kanisa lake lilijaa na wasikilizaji, watu maarufu, wenye elimu na wageni wanaokuja Geneva. Hivyo ndivyo Injili ilivyoenezwa. Gaussen akitiwa moyo na hayo aliyochapisha masomo yake, akiwa na nia ya kuanzisha mafunzo ya unabii. Baadaye alikuwa mwalimu katika chuo kimoja na kila jumapili aliendelea na mafunzo ya katekismu, akiwafundisha watoto maandiko Matakatifu. Mafundisho yake yaliyotolewa kwa kinywa na kuandika mambo kwa njia ya kuchapa. Na kama mwalimu wa watoto wa muda mrefu aliwafundisha watu juu ya kurudi kwa Yesu kulikoa karibu.TU 175.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents