Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wahubiri Watoto wa Scandinavia

  Huko Scandinavia pia ujumbe wa marejeo ulihubiriwa. Wengi waliongoka na kuzitupilia mbali njia zao mbaya, wakataka rehema na msamaha wa Kristo. Lakini wenye dini ya kawaida ya jumla waliwapinga waongofu wenye dini hawa, na baadhi ya wahubiri hao walitupwa kifungoni. Wakafika mahali pengine ambapo wahubiri wa marejeo ya Kristo walinyamazishwa hivyo, Mungu aliwatumia watoto wadogo kuhubiri. Kwa kuwa walikuwa wadogo serikali haikuweza kuwachukulia hatua yoyote.TU 175.3

  Katika nyumba za watu ndimo watu walikuwa wakikutana ili kusikia ujumbe wa marejeo. Baadhi ya watoto hao waliokuwa wakihubiri umri wao ulikuwa miaka sita au minane. Walipokuwa wakishuhudia juu ya upendo wa Mwokozi, maisha yao yalikuwa ya kawaida kwa watoto wa umri huo. Waliposimama kuhubiri hali yao ilikuwa tofauti na hali ya kawaida. Nguvu ya pekee ilikuwa ndani yao. Walitoa maonyo kwa uthabiti wa pekee. Walisema kwa ujasiri, “Mcheni Mungu na kumtukuza, maana saa ya hukumu yake imekuja”TU 175.4

  Watu walisikia maonyo haya kwa hofu na kutetemeka. Roho wa Mungu aliwazungumzia. Wengi walilazimika kuyachunguza maandiko kwa makini, wakasahihisha njia zao. Kazi ilifanyika mpaka wakuu wa serikali wakakiri kuwa mkono wa Mungu ulikuwa ukiwaongoza.TU 176.1

  Yalikuwa mapenzi ya Mungu kwamba habari za kurudi kwa Kristo zihubiriwe katika Scandinavia, kwa hiyo aliwawezesha watoto ili wafanye kazi hiyo. Wakati Yesu alipokaribia Yerusalemu, watu walitishwa na makuhani na watawala ili wanyamaze ama wasishangilie, Yesu anapoingia mjini. Lakini watoto katika hekalu walipaza sauti zao na kuimba “Hosana Mwana wa Daudi”. Mathayo 21:8-16. Jinsi Mungu alivyowatumia watoto katika kuja kwa Kristo mara ya kwanza, hali kadhalika atawatumia kutangaza kurudi kwake mara ya pili.TU 176.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents