Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Andiko Rahisi Huleta Uthibitisho

  Wahubiri waliweka shoka kwenye mashina ya miti sawa na Yohana Mbatizaji alivyofanya, na kuwahimiza watu kuuza matunda yapasayo toba. Maneno ya ushuhuda kwamba hali ya toba imepatikana, yalisikika yakisemwa dhahiri na wahubiri mimbarani waziwazi. Wengi walimtafuta Bwana kwa moyo wa toba halisi. Anasa za dunia zilizowajalia kwa muda mrefu sasa waliziachilia mbali, na kutafuta yale ya mbinguni. Walijiunga kutangaza kwa moyo wote, kwamba, “Mcheni Mungu na kumtukuza kwa maana saa ya hukumu yake imekuja”TU 177.1

  Wenye dhambi walijuta kwa machozi, na kuuliza, “Je, tufanye nini ili tupate kuokoka?” Watu ambao waliishi katika hali ya ufedhuli, wakatafuta jinsi ya kurekebisha hali zao. Wale waliopata amani katika Kristo walikuwa na hamu kuu ya kuwaelezea wengine ili nao wapate amani hiyo. Mioyo ya wazazi iligeukia kwa watoto wao, na ya watoto kwa wazazi wao. Malaki 4:5-6. Vizuizi viletwavyo na kiburi na kutakabari viliondolewa mbali. Mioyo ya maungamo ilikuwa dhahiri kwa wote. Kila mahali watu walikuwa wakimlilia Mungu. Wengi alikuwa wakiomba usiku kucha ili kuhakikisha kuwa wamepata msamaha kwa ajili ya dhambi zao.TU 177.2

  Watu wa hali zote, wakubwa kwa wadogo, wenye elimu na wasio na elimu, matajiri kwa maskini walikuwa na hamu ya kusikia ujumbe wa kurudi kwake Yesu. Roho wa Mungu aliwezesha ujumbe huu utangazwe kwa nguvu. Katika mikutano yote malaika watakatifu walikuwamo na waumini wakazidi kuja kwa Bwana kila siku. Makutano makubwa yalikuwa yakikutana na kukaa kimya ili kusikiliza ukweli huu. Mbingu na nchi zilionekana kukutana. Watu walirudi nyumbani kwao wakijaa furaha na kuyatafakari yote yaliyosemwa usiku kucha. Mtu aliyehudhuria mikutano hiyo hakuweza kuisahau.TU 177.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents