Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ujumbe Ulipangwa

  Kutangaza kwa wakati hasa wa kuja kwa Kristo kulipingwa na watu wote, tangu wachungaji mpaka wenye dhambi. Wengi walisema kuwa hawapingi fundisho la kurudi kwake Yesu, ila wanapinga ule muda hasa wa kurudi kwake. Lakini macho ya Mungu yalisoma mioyo yao. Hawakutaka kusikia kuwa Mungu atakuja kuuhukumu ulimwengu kwa haki. Kazi zao zilikuwa mbovu, na zisingeweza kusimama katika hukumu ya Mungu. Hawakuwa tayari kukutana naye, sawa kama Wayahudi hawakuwa tayari kumkaribisha Yesu alipokuja mara ya kwanza. Hawakutaka kusikia ujumbe wa Biblia tu, bali waliwadhihaki wale waliokutazamia kurudi kwake. Shetani alimdhihaki Kristo, kwamba watu wake hawataki arudi. Wale waliokuwa wanapinga ujumbe walisema kuwa, “Hakuna ajuaye saa ya kuja kwake”. Andiko linasema, “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna ajuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake”. Mathayo 24:36. Elezo hilo dhahiri lilielezwa na wale waliokuwa wakikungojea kurejea kwa Bwana, lakini wale wapingaji walipotosha maana yake.TU 177.4

  Mmoja alisema kuhusu Mwokozi kwamba lazima asingemharibu mtu. Ingawa hakuna ajuaye wakati wa kuja kwake, tunapaswa kujua anapokaribia. Tusipojishughulisha kujua itakuwa bahati mbaya kwetu kama ilivyokuwa kwa wote wa ulimwenguni, wakati wa siku za Nuhu. Kristo alisema, “Usipokesha nitakuja kwako kama vile mwizi ajavyo, nawe hutaijua saa nitakayokuja kwako.” Ufunuo 3:3.TU 178.1

  Paulo anasema kwa wale wenye kujali maonyo, “Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwizi. Ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana” 1Tes. 5:2-5.TU 178.2

  Lakini wale wanaotafuta udhuru wakiziba masikio wasiyajali maonyo yale maneno, “Hakuna ajuaye siku wala saa”, huendelea kugonga kwao kama mwangwi, hata kwa wafuasi ya Kristo pia. Kadiri watu walivyokuwa wakiutafuta ukweli, wapotofu hawa waliingilia na tafsiri potofu ili kuwapotosha.TU 178.3

  Watu wanyofu katika kanisa walikuwa wa kwanza kupokea ujumbe. Pale watu walipotawaliwa na waongozi wao, na pale watu wanapochunguza Maandiko kupambanisha andiko na andiko.TU 178.4

  Wengi walipotezwa na waume, wake, wazazi, watoto hata ikaonekana kana kwamba ni dhambi hata kwenda kusikiliza tu. Ujumbe wa marejeo ukahesabika kana kwamba ni uzushi. Malaika waliagizwa kuwalinda waaminifu hawa, ili waendelee mpaka nuru zaidi ifunuliwe kwao, kutoka katika kiti cha Mungu.TU 179.1

  Watu waliupokea ujumbe wa marejeo walikesha na kukungojea kurudi kwake Bwana, maana muda uliokuwa ukitazamiwa ulikuwa umekaribia. Waliingoja saa hii kwa utulivu na kicho hasa. Katika kundi hilo lililokuwa likingojea, hakuna awezaye kusahau hali waliyokuwa nayo. Kwa muda wa majuma kadhaa kabla ya muda huo shughuli zote za kidunia ziliachwa kabisa. Waumini walijichunguza mioyo yao kwa uangalifu sana, kwa vile baada ya wakati mfupi tu wangeicha dunia hii. Hapakuwa na utengenezaji wa mavazi ya kuvaa wakati wa kupaa, lakini wote walikuwa na tunu ya milele ya kumwona Bwana. Usafi wao haukuwa wa mavazi, bali wa mioyo, tabia iliyotakaswa kwa damu ya Kristo. Je, wangaliko watu wa Mungu namna hiyo, waaminifu wanaotafuta utakaso wa namna hiyo?TU 179.2

  Mungu alitaka kuwajaribu watu wake. Mkono wake ulifunika kosa katika kuhesabu tarehe katika unabii. Wakati wa kurejea kwa Kristo, (yaani katika mwaka 1844) ukapita bila Kristo kurudi. Hivyo, wale waliotazamia Mwokozi wakati huo walipata uchungu na masikitiko yasiyoelezeka. Wakati Mungu alikuwa akiwajaribu wale walikuwa wakingojea, ambao ni wafuasi wake. Wengi walikuwa wamevutwa kujiunga kwa njia ya hofu tu. Hawa walisema kuwa hawakuamini kuwa Yesu angerudi kwa wakati huo. Walakini walikuwa kati ya kwanza kuwadhihaki waaminifu wa kweli.TU 179.3

  Lakini ni Yesu na mbingu yote ndiyo waliwahurumia watu wake. Kama pazia lingefunuliwa wangeweza kuona jinsi malaika wanavyowashughulikia kwa upendo usiosemeka, ili wasikumbwe na gharika ya shetani.TU 179.4

  Marejeo: TU 179.5

  Travels and Adventures of Rev. Joseph Wolff, Vol. 1 pp. 6-7. TU 179.6

  Joseph Wolff, Researches and Missionary Labour, pp. 404 -405. TU 179.7

  Journal of the Rev. Joseph Wolff, p. 96 TU 179.8

  W.H.D Adams, In Perills Oft. Pp. 192, 201 TU 179.9

  Journal of the Rev. Joseph Wolff, pp. 377, 389 TU 179.10

  L. Gaussen Daniel the Prophet — Vol. 2 preference.TU 179.11

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents