Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  21/Kuvuna Upepo wa Kimbunga

  William Miller na wenzake walitaka kuamsha wataalamu wa dini ili wasimame katika tumaini la imani ya kweli na ukristo halisi wa kanisa. Walishuhgulika pia na kuwaongoa wale wasiokuwa na imani wapate kutubu na kuungama. Wao hawakujishughulisha na habari ya madhehebu, walichotaka ni kuona watu wanasimama katika ukweli halisi. Miller alisema “Nataka kufaidia kila mtu bila kujali ni wa dhehebu gani”. Kama wakristo watakufurahia kurudi kwa Kristo litakuwa jambo muhimu. Hata wale wasiouona umaana wake sina la ziada kwao. Wala sina nia ya kutenganisha mikutano. Wengi wa walioongolewa nami waende kujiunga na makanisa tofauti, tu bora wawe waongofu halisi.TU 180.1

  Lakini waongozi wa makanisa walitenga wale walioamini ujumbe wa marejeo. Waumini waliyapenda makanisa yao. Lakini walipoona kuwa inawapasa kuchunguza unabii, walikataliwa. Lakini kwa ajili ya uaminifu wao kwa Bwana walikubali kutengana na makanisa hayo. Katika mwaka 1844 watu kiasi cha hamsini elfu walijitenga na makanisa hayo.TU 180.2

  Katika makanisa mengi kumekuwako ongezeko la kawaida za kidunia zikiingia taratibu, na hizo hudhoofisha mambo ya kiroho. Lakini katika mwaka huo kulionekana hali ya badiliko katika makanisa yote nchini. Hayo yalithibitishwa kwa kusemwa kanisani na kuandika magazetini.TU 180.3

  Mchungaji Barnes, Mwandishi wa Komentari na kiongozi wa makanisa ya Philadephia alisema kwamba “….. sasa hakuna mwamko, hakuna uongofu, hakuna kukua kwa neema katika uongozi, wala hakuna wasiwasi kuhusu kuongoa watu na kuwaleta katika wokovu.” Kuna maongezeko ya anasa za kidunia kanisani. Na hayo yanakumba madhehebu yote.TU 180.4

  Katika mwezi wa Februari mwaka ule ule, Mwalimu Finney wa Oberlin College, alisema, “Kwa jumla makanisa ya Kiprotestanti katika nchi yetu, yamefifia sana na kuwa na hali ya uadui katika msimamo wake. Hali ya kiroho imefifia mno kiasi cha kutisha. Washiriki wake wameingia katika hali mbaya sana, kumebakia kufuata mitindo tu. Wameungana na walimwengu kwa hali zote za kianasa na siku za ulafi na starehe. Makanisa yanaendelea kuzama uovuni kwa namna ya kutisha. Yamejitenga mbali sana na Bwana, naye Bwana ameondoka kati yao”TU 180.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents