Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jinsi Sabato “Ilivyobadilishwa”

  Unabii unaeleza kuwa, Upapa utafikiri kubadili “Wakati na Sheria” Daniel 7:25. Ili kusudi kuimarisha ibada ya sanamu, heshima ya kuwakumbuka wafu na sura zao iliingizwa katika kanisa la Kikristo. Tamko la baraza lao kuu kwamba, mifano au picha za watu mashuhuri ziwekwe ili kuwakumbuka, lilithibitisha ibada ya sananu. Kwa njia hiyo Rumi ikathubutu kufuta amri ya pili katika amri za Mungu, ambayo inakataza kuabudu sanamu, halafu wakagawa amri ya kumi kuwa amri mbili ili hesabu ya amri iwe kamiliTU 15.2

  Viongozi wa kanisa ambao ni wapotofu, wakageuza amri ya nne, wakaondoa Sabato ya siku ya saba, siku ambayo Mungu aliibariki na kuitakasa (Mwanzo2:2-3), badala yake “wakatukuza siku ya jua” ambayo ilikuwa ikitukuzwa na wakafiri. Katika karne ya kwanza siku ya Sabato ilikuwa ikitukuzwa na wakristo wote. Lakini shetani alijitahidi kutimiza makusudi yake mapotofu, ndipo kutukuza Jumapili kulianza (siku ya jua) eti kuadhimisha siku ya ufufuo wa Kristo. Ibada za kidini ziliadhimishwa sasa hiyo kama kumbukumbu ya ufufuo wa Kristo. Walakini Sabato iliendelea kutumzwa kama siku Takatifu.TU 15.3

  Shetani aliwaongoza Wayahudi kuitilia Sabato vikwazo vingi mpaka ikawa mzigo. Na sasa kwa mpango huu mpya aliougundua wa kutukuza siku ya ufufuo, alitupa laumu kwa Wayahudi kwamba Sabato ni ya Kiyahudi, wakati wakristo walikuwa wanafurahia siku ya ufufuo. Aliwaelekeza watu waone kuwa Sabato ya siku ya Saba ni ya huzuni na masikitiko tu, kwa hiyo haifai. Hii ilikuwa chuki kwa Wayahudi.TU 15.4

  Mfalme Constantine aliamua kuwa Jumapili iwe siku ya kupunzika katika Dola yake yote. Siku ya jua ilitukuzwa na watu wake ambao ni wapagani, na wakristo pia wakaitukuza. Makasisi wa makanisa wakatilia mkazo amri hiyo maana ndio waliomshauri mfalme atoe amri hiyo. Makasisi kwa kutaka vyeo walidhani kuwa kama watu wote, wakafiri na wakristo pia wakiitukuza siku hiyo ya jua, ukuu wa kanisa utaenea na kuwa na mvuto zaidi. Lakini watu wa Mungu waliendelea kutukuza Sabato ya kweli, ingawa walianza polepole kuitukuza Jumapili kama ilivyoamriwa na mfalme.TU 16.1

  Mchanganyaji mkuu alikuwa hajamaliza kazi yake bado. Alijihusisha kabisa katika kutumia uwezo wake kwa njia ya naibu wake mwenye kiburi anayejidai kuwa wakili wa Kristo (Papa). Halmashauri kubwa zilifanyika ambazo ziliidhinisha cheo hicho na kukitangaza ulimwenguni pote. Karibu kila baraza lililofanyika, Sabato ilishambuliwa kidogo, na jumapili ilitukuzwa. Hivyo sikukuu ya kipagani mwishowe ikapewa heshima kama siku ya Mungu, na Sabato ya Mungu ikatajwa kuwa ni siku ya Wayahudi kwa hiyo ikatajwa kuwa ni siku ya Wayahudi, kwa hiyo ikapigwa marufuku.TU 16.2

  Uasi ukafaulu kujitukuza kama “Mungu na kuabudiwa” 2 Thes. 2:4. Amethubutu kubadili amri ya Mungu inayomtaja Mungu kuwa Mungu wa kweli aliye hai. Katika amri ya nne Mungu anadhihirishwa kwamba ni Muumba. Siku ya saba ya juma ilitakaswa na kutengwa kuwa siku ya kupumzika kwa wanadamu, ikimkumbusha kwamba Mungu ndiye muumbaji na siku hiyo ndiyo ya kuabudu. Shetani alijitahidi kumgeuza mwanadamu asiitii sheria ya Mungu na kwa hiyo shambulio lake, lilielekezwa kwa amri ya nne ambayo inamtaja Mungu kuwa Muumbaji.TU 16.3

  Sasa Waprotestanti husema kwamba ufufuo wa Kristo siku ya Jumapili, huifanya siku hiyo iwe Sabato ya Kikristo. Lakini hakuna heshima ya namna hiyo iliyotolewa na Yesu au mitume. Utunzaji wa Jumapili ulianzia kwenye “Siri ya kuasi”. (2Thes. 2:7) ambayo ilianza kuonekana hata siku za Paulo. Itatolea sababu gani ya badiliko kama hilo, ambalo halikuidhinishwa na Biblia?TU 16.4

  Katika karne ya sita askofu wa rumi alitajwa kuwa kichwa cha kanisa lote. Ukafiri umeingiza upapa. Joka amempa mnyama “uwezo wake na kiti chake, na mamlaka kuu” Ufu. 13:2.TU 16.5

  Sasa imeanza miaka 1260 ya mateso ya mapapa ambayo ilitabiriwa na Unabii wa Danieli 7:25 na Ufunuo 13:5-7. Wakristo walilazimika kuchagua moja kati ya mambo mawili. Kukana Imani yao na kukubaliana na mipango ya ibada ya Rumi; au kuteseka vifungoni na kupoteza maisha yao. Sasa maneno ya Yesu yalitimia, yasemayo: “Mtasalitiwa na wazazi, na ndugu na jamaa na marafiki; na baadhi yenu mtauawa. Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu” Luka 21:16-17.TU 17.1

  Dunia ikawa uwanja wa vita. Kwa miaka mamia kanisa la Mungu lilikuwa katika msukosuko mkuu. Watu wakawa wakiishi mafichoni tu. “Mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengezwa na Mungu, ili wamlishe huko Muda wa siku elfu na mia mbili na sitini” Ufunuo 12:6TU 17.2

  Kule kutawala kwa kanisa la Kirumi kuliko wa mwanzo wa wakati wa Giza. Imani kwa Kristo ilihamishiwa kuwa kwa papa wa Rumi. Badala ya kumtegemea Kristo mwana wa Mungu kuwa ndiye mwondoa dhambi, na mwenye uzima wa milele, watu watalazimishwa kwa papa wa Rumi na kwa maaskofu ambao papa amewapa mamlaka. Papa alikuwa ndiye mwombezi wao. Kwao alikuwa kama Mungu. Mtu aliyepinga maongozi yake alistahili hukumu. Kwa njia hiyo mawazo ya watu waligeuzwa upande, kutoka kwa Mungu kuelekea kwa binadamu mwenye dhambi, aliye katili, na kwa mkuu wa giza mwenyewe ambaye hutumia uwezo wake kuwapotosha. Wakati maneno matakatifu ya Biblia yanapoachwa, mtu hujivuna na kujitukuza na kutumbukia katika upotofu.TU 17.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents