Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Umoja wa Ulimwengu

  Makanisa mengi ya Kiprotestanti yamefuata mfano wa Rumi kwa kuungana na “wafalme wa dunia” — makanisa na serikali kwa uhusiano wao na serikali za kidunia na madhehebu mengine kwa kutafuta kupendelewa na dunia. Neno Babeli — machafuko — linaweza kuhusisha makanisa haya yanayodai kupata mafundisho yao kutoka katika Biblia, na hali bado yanagawanyika katika vidhehebu vingi mno ambavyo vinapingana kwa mafundisho.TU 184.2

  Kazi ya kanisa la Kirumi, lasema kwamba “Kama kanisa la Rumi lilipata kuwa na hatia ya kuabudu sanamu kwa kuhusu watakatifu, binti yake kansia la Anglikani linasimama kwa hatia ile ile, ambalo lina makanisa kumi yaliyojitoa kumwabudu Maria kwa moja lilijitoa kwa Kristo.”TU 184.3

  Na pia Dr. Hopkins atangaza, “Hakuna sababu ya kufikiri roho ya kumpinga Kristo na kujizoeza kushikamana kwa kile ambacho sasa kinaitwa kanisa la Roma tu. Makanisa ya Kiprotestanti yanampinga ndani yao na yako mbali sana na matengenezo sahihi kutoka katika uasi na ufisadi.”TU 185.1

  Kuhusu kujitenga kwa kanisa la Presbyterian kutoka Rumi, Dr. Guthrie aliandika, “Miaka mia tatu iliyopita, kanisa letu lilijitenga na Rumi, likishikilia Biblia katika mikono yake na likiwa na neno kuu lisemalo, ‘Chunguza maandiko’ Halafu aliuliza swali hili, ‘Je, walitoka Babeli wakiwa safi?’”TU 185.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents