Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Upotovu wa Kwanza Kutoka Katika Ukweli wa Injili

  Je, kanisa lilifarakana jinsi gani na usafi wa Injli? Lilifarakana kwa njia ya kujiunga na ukarifi, na kushusha kanuni za ukristo ili iwe rahisi wakafiri kujiunga na kanisa. Kuelekea mwisho wa karne ya pili makanisa mengi yalikuwa na umbo jingine kabisa. Wanafunzi wa kwanza walipomalizika na kulala makaburini, watoto wao pamoja na waongofu wapya wakafuata njia nyingine “Desturi za kikafiri zikafurikia ndani ya kanisa, na sanamu zikahalalishwa Ukristo ukategemea msaada wa serikali. Ukristo wa jina tu ukakubaliwa na wengi. Lakini wengi waliendelea kuwa wakafiri tu, wakizidi kuabudu sanamu kwa sirisiri”TU 185.3

  Je, mambo yayo hayo hayakurudiwa rudiwa karibu yote ya watu wanaojiita Waprotestanti? Kadiri watangulizi wa kweli walivyokufa, ndivyo walivyofuata walivyogeuza njia. Wakawa vipofu kabisa wasipokee ukweli uliopokelewa na baba zao. Wakawa kana kwamba sio wana wa watengenezaji, wakijitenga na kujikana nafsi na kuacha ulimwengu.TU 185.4

  Lo, makansia yamejitenga na ukweli wa Biblia kiasi gani! John Wesley alisema, kuhusu fedha, “Usipoteze sehemu yoyote ya talanta ya thamani ….. kwa mapambo na kujirembesha. Wala usipoteze muda kupamba nyumba yako, na vitu vya thamani, na mapicha na maridadi za kila namna. Lakini uridhike na heshima itokayo kwa Mungu.”TU 185.5

  Mtawala, wana siasa, madaktari, wanasheria, wafanya biashara, wote walijiunga na kanisa kama washriki, ili iwe njia ya kuendeleza mambo yao ya ulimwengu. Halimashauri za kanisa zilikuwa zikiongozwa na makafiri hao ambao walijifanya kana kwamba ni waongofu wa kweli, huku wakitafuta anasa za ulimwengu. Makanisa makubwa, maridadi sana yalijengwa. Wachungaji hodari, ambao kazi yao hasa ilikuwa kuwaburudisha watu, walikuwa wakilipwa mishahara mikubwa sana, mahubiri yao yalikuwa ya kuwaburudisha tu wasikilizaji. Hivyo dhambi zilifichika chini ya uongofu wa mfano tu.TU 185.6

  Dhambi kuu iliyoshitaka dhidi ya Babeli ni kwamba “uliwafanya mataifa kunywa mvinyo wa ghadabu ya mafundisho ya uongo yanayokubalika na Babeli kama mvuto wake wa kupotosha juu ya dunia kwa kufundisha mafundisho yapingayo matamshi ya kweli ya Biblia.”TU 186.1

  Ingekuwa siyo dunia kulewa na mvinyo wa Babeli, maelfu ya watu wangesadikishwa na kuongolewa na ukweli halisi wa Neno la Mungu. Lakini imani ya dini huonekana kuvurugwa na kutolingana kiasi cha kuwafanya watu kutofahamu cha kuamini. Dhambi ya ugumu wa moyo wa dunia imesimama mlangoni mwa kanisa.TU 186.2

  Marejeo: TU 187.1

  Bliss p. 328 TU 187.2

  Congregation Journal, Mei 23, 1844. TU 187.3

  Richard Challoner, The Catholic Christian Instructed, Preface, pp. 21-22 TU 187.4

  Samuel Hopkins, “A Treatise on the Millenium” Works, Vol 2, p. 328.TU 187.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents