Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ukakamavu Kidini Waonekana.

  Wakati ule ushupavu kidini ulionekana. Baadhi yao walionekana kuwa na msimamo mwingine mwingine. Mawazo yao ya aina nyingine ya kishupavu hayakukubaliwa na wengine wa imani ya marejeo. Mambo yao yalileta shutuma kwa ukweli wa marejeo.TU 189.4

  Shetani alikuwa akipoteza raia zake walioongolewa katika imani ya marejeo, kwa hiyo alileta machafuko katika waumini, kiasi kwamba wengine walipita kiasi. Alikuwa tayari kutafuta vikasoro vyo vyote na kuvifanya viwe ndiyo sababu ya kulaumu msimamo wa watu wa marejeo. Kadiri alivyowashawishi watu wengi waonekane kana kwamba wameongoka na kujiunga na ujumbe wa marejeo ndivyo walivyofanikiwa.TU 189.5

  Shetani ni “mshitaki wa ndugu”. Ufunuo 12:10. Malaika zake wako tayari kuona kasoro za watu wa Mungu ili kuzishika na kutoa lawama kubwa. Wakati huo wema wote wa uteule wa watu wa Mungu hausemwi.TU 190.1

  Katika historia yote ya kanisa hakuna matengenezo yo yote yaliyofanywa bila kuingizwa ili kuvuruga. Pale Paulo alipoanzisha kanisa, baadhi ya wale waliojidai kuwa waumini walionekana kuingiza maneno ya uzushi. Luther pia alisumbuliwa na watu wa jinsi hiyo, ambao walikuwa wakijidai kuwa Mungu amewaagiza kufanya vile na vile, watu ambao walitegemea maoni yao badala ya maandiko matakatifu. Wengi walidanganywa na waalimu wa namna hii na kujiunga na Shetani kuharibu kazi ya Luther aliyoambiwa na Mungu. Wesley alipambana na hila za Shetani kwa kuwasukuma watu ambao hawakuwa na utaratibu, wala si waongofu ila walikuwa washupavu tu wakitaka mawazo yao yafuatwe na kila mtu.TU 190.2

  William Miller hakuwahurumia watu wa aina hiyo ya ushupavu katika dini. Alisema, “Mwovu anao uwezo mkuu juu ya baadhi ya watu wa siku hizi”. Mara nyingi nimeshuhudia ukristo wa mtu wa kweli, rohoni mwake, na usemi wake kuliko kelele zote zinazopigwa na wakristo.TU 190.3

  Wakati wa Matengenezo, maadui walitupa lawama juu ya watu waliokuwa na juhudi mno kuyapinga kwamba ni washupavu. Hali ile ile ilionekana katika kuwapinga watu wa marejeo. Wala hawakuridhika na kuyasema makosa yao tu, lakini walieneza uvumi ambao sio kweli. Walichafuliwa na kule kumtangaza Kristo kuwa yu karibu. Waliogopa, isije ikawa ni kweli, lakini alitumaini kuwa si kweli. Hii ndiyo iliyokuwa siri ya vita yao na watu wa marejeo.TU 190.4

  Kuhubiriwa kwa ujumbe wa malaika wa kwanza kulielekea kukomesha ushupavu. Wale waliokubaliana na kundi hili walipatana, wala haikuweko tofauti yoyote. Walipendana, na walimpenda Yesu, ambaye walitazamia kumwona karibuni. Imani yao moja ya tumaini moja viliyakinga mashambulio ya Shetani.TU 190.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents