Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Makosa Yalisahihishwa.

  “Na Bwana arusi alipokawia wote walisinzia, wakalala”. Lakini usiku wa manane palikuwa na kelele, “Haya bwana arusi anakuja, ondokeni kwenda kumlaki” katika mwaka wa 1844 ujumbe ulitangazwa kwa maneno yale yale ya Biblia.TU 190.6

  Kilichoonyesha kuwa huu ndio wakati wa tangazo hilo kutolewa na kundi hilo kuunganika pamoja na kule kugunduliwa kwa amri ya Artashasta ya kuujenga na kuurudisha mji wa Yerusalemu, ambayo ndiyo mwanzo wa muda wa miaka 2300 ya unabii, iliyotukia katika B.C 457. Haikutokea mwanzo wa mwaka kama ilivyoaminiwa, bali ni katika miezi ya Septemba, Oktoba na Novemba, yaani robo ya tatu ya mwaka. Kwa hiyo kuhesabu kutoka 457 B.C miaka 2300 itamalizika mwaka 1844 robo ya tatu ya mwaka. Anguko la Kale pia hutaja robo ya tatu ya mwaka kama ndiyo siku ya upatanisho katika habari za ukuhani, na siku ya kutakasa patakatifu.TU 191.1

  Kule kuchinja kondoo wa pasaka kulikuwa kivuli cha kifo cha Kristo, kitakachotimia kwa wakati wake, katika tarehe ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza wa Kiyahudi, ambayo kwa karne nyingi palikuwa pakichinjwa kondoo wa pasaka, Kristo aliianzisha siku kuu ya kukumbuka kifo chake, kama “mwanakondoo wa Mungu” Usiku ule ule alikamatwa ili akasulubiwe na kuchinjwa.TU 191.2

  Hali kadhalika kivuli cha kuhusika na kurudi kwa Kristo budi kitimilike. Kwa wakati ulioamriwa kwa njia ya mfano. Kutakaswa kwa patakatifu, au siku kuu ya upatanisho iliyokuwa ikitokea katika siku ya kumi ya kila mwezi wa saba ya Kiyahudi, ambayo Kuhani mkuu alifanya upatanisho kwa Waisraeli wote, na kuondoa dhambi zao zote kutoka mahali patakatifu, watu walitakasika. Ndivyo hivyo ilivyoaminiwa kuwa Kristo pia atatokea ili kuitakasa dunia kwa njia ya kuiangamiza dhambi pamoja na wenye dhambi, na kuwachukua watu wake. Siku ya kumi ya mwezi wa saba, ambayo ni siku ya upatanisho, wakati wa utakaso wa patakatifu, ambapo katika mwaka 1844 ilikuwa Oktoba 22, ilihesabiwa kuwa ndiyo siku ya kurudi kwake Kristo, miaka 2300 ingemalizika mwaka 1844. Kwa hiyo ikakubaliwa kuwa wakati huo ndio wa kurudi kwa Kristo.TU 191.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents