Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kilio Cha Usiku Wa Manane

  Hoja hizo zilikuwa kubwa kiasi cha kuwasadikisha watu, na mahubiri yakatolewa, yale yajulikanayo kuwa ni “kilio cha usiku wa manane” Watu maelfu wakajiunga kuyatoa, hali ya ushupavu wa dini iliendelea kutoweka sawa na ukungu wakati wa mapambazuko. Mambo yakaenea kwa upesi, sawasawa na mawimbi, toka mji hata mji, na toka kijiji hata kijiji. Kazi ikafanana na ile ya wakati wa uamsho katika Israeli, baada ya kudidimia dhambini. Kulikuwa na mwamko mkubwa sana, maungamo ya dhambi na kujichunguza mioyo. Waliachilia mbali anasa za dunia wakaambatana na uongofu wa kweli.TU 191.4

  Katika madhehebu yote tokea siku za mitume hakuna dhehebu lililokuwa huru kutoka katika dhambi na katika mwaka 1844.TU 192.1

  Kama vile katika mwito “Bwana arusi anakuja, walingojea, waliamka wakaanza kuzitengeneza taa zao.” Ndivyo watu walivyoamka kuchunguza maandiko kwa bidii sana. Watu wa kawaida tu ndio walioitikia mwito mara ya kwanza, wala sio watu wataalamu. Wakulima waliacha mavuno yao mashambani, mafundi wakaacha vyombo vyao, wote wakaondoka kwenda kulitangaza neno la Mungu. Kwa kawaida makanisa hayakujali ujumbe huu, na wale walioupokea walifutwa katika makanisa hayo. Wale wasioamini walikuja kujiunga na watu wa marejeo waliona kuwa kuna uwezo mkuu katika ujumbe huu. “Haya! Bwana arusi yuaja” Imani ilileta jawabu kwa maombi.TU 192.2

  Kama manyunyu ya mvua yanavyokuwa chini, hali kadhalika na neema ya Mungu ilivyokuwa kwa wale waliokuwa wakiutafuta ukweli. Wale waliotumaini kusimama mbele ya Mwokozi karibuni alikuwa na furaha isiyo kifani. Roho Mtakatifu aliyeyusha mioyo yao.TU 192.3

  Wale walioupokea ujumbe walitazamia wakati wa kukutana na Bwana wao. Waliombeana sana. Kila mara walikutana faraghani kuzungumza na Bwana, na sauti za waombaji hawa zilipaa juu kutoka kila mahali. Walihitaji Mwokozi zaidi ya chakula chao. Wakati wo wote walipokuwa na shaka lolote, hawakutulia mpaka waone uthibitisho juu ya jambo hili, hasa msamaha wa dhambi zao.TU 192.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents