Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uchungu Tena

  Lakini tena wakati waliomtazamia Mwokozi ulipita, na Mwokozi hakutokea. Sasa wakawa kama Mariamu alivyokuwa alipokwenda kaburini walikomzika Yesu. Alipofika huko asiuone mwili wa Yesu, alianza kulia huku akisema, “Wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka” Yohana 20:13.TU 192.5

  Waliogopa kwamba wasioamini watazidi kuhakikisha kuwa ujumbe wao sio wa kweli. Lakini hakuna dalili kuwa ujumbe wao sio wa kweli. Lakini hakuna dalili ya ghadhabu ya Mungu iliyotokea, basi waliendela tu kuvumilia mizaha na mashutumu. Watu wengi walioamini walitupilia mbali imani yao, na kurudi nyuma. Wenye mizaha walifaulu kuvuta wenye mashaka na waoga kuacha msimamo waliokuwa nao. Wote hawa walijiunga na kusema kuwa ulimwengu utaendelea kuwa kama ulivyo kwa miaka maelfu.TU 192.6

  Waumini wa kweli walikuwa wametoa mali zao zote kwa ajili ya Kristo, na kama walivyoamini, walikuwa wametoa maonyo ya mwisho kwa walimwengu huku wakiomba na kutumaini kurudi kwa Bwana, wakisema, “Naam, na uje Bwana”, na sasa Bwana hakuja. Basi kuanza maisha upya, na kukabili mizaha ya walimwengu juu yao, lilikuwa jaribu lisilowezekana kuchukulika.TU 193.1

  Wakati Yesu alipoingia Yerusalemu kwa shangwe, wafuasi wake waliamini kuwa alikuwa tayari kukikalia kiti cha enzi cha Daudi, na kuwaokoa watu wake mikononi mwa watesi wao. Kwa matumaini na shangwe kuu, wengi walitandika nguo zao njiani ili apite na kukanyaga juu yake, na wengi walibeba matawi ya mitende kufurahia tukio hilo. Wanafunzi walikuwa wakilitimiza shauri la Mungu, lakini walishangazwa na kuingia uchungu kwa yaliyotokea. Walakini baada ya muda mfupi waliyashuhudia mateso ya Kristo na kifo chake, wakamzika kaburini. Matumaini yao yalikufa pamoja na Yesu. Hawakuelewa mpaka Bwana alipofufuka ndipo wakafahamu kuwa yote yalitabiriwa na manabii.TU 193.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents