Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Patakatifu Pa Patakatifu Mno.

  Katika patakatifu palikuwamo kinara cha taa upande wa kusini pamoja na taa zake saba zikiwaka mchana na usiku. Upande wa kaskazini ilikuwako meza ya mikate ya wonyesho. Mbele ya pazia linalotenganisha patakatifu na patakatifu mno, palikuwako madhabahu ya uvumba ulifukizwa kila siku moshi ukipaa pamoja na sala za Waisraeli, mbele za Mungu.TU 197.1

  Katika patakatifu mno lilikuwamo sanduku lililonakishiwa kwa dhahabu ambalo lilikuwa likitunza amri kumi za Mungu. Juu ya sanduku kulikuwa na kiti cha rehema kikikabiliwa na makerubi wawili walioumbwa kwa dhahabu. Katika chumba hiki kuwako kwa Mungu kulionekana daima kati ya makerubi. Baada ya Waebrania kukaa Kanani, hema takatifu ilibadilishwa na hekalu lilijengwa na Sulemani, ambayo ingawa ilikuwa jengo la kudumu na kubwa lilifanya kazi ile ile ilikuwa na mfano ule ule; mpaka ilipobomolewa siku za akina Daniel ….. mpaka maangamizo yake na Warumi katika mwaka 70 Ad. Hii ndiyo hema takatifu duniani ambayo tunasoma habari zake katika Biblia. Hema takatifu ya agano la kale. Lakini je, agano jipya haina hema takatifu?TU 197.2

  Msomaji na mtafutaji ukweli akifungua kitabu cha Waebrania huona kuwa agano jipya, au agano la pili huzungumzwa katika maneno hayo yaliyosemwa hapo kwanza “hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida zake na ibada, na patakatifu pake pa kidunia”. Tukigeukia kusoma sura iliyopita twasoma, “Basi katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili”, “Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni, mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu” Waebrania 8:1-2.TU 197.3

  Hapa ndipo inafunuliwa hema takatifu ya agano jipya. Hema takatifu ya agano la kwanza ilifanywa na Musa, hii ya sasa imefanywa na Bwana. Katika hema ya kwanza waliohudumu ni makuhani wa kidunia, katika hii ya pili, Kristo kuhani wetu Mkuu huhudumu akiwa upande wa mkono wa kuume wa Mungu. Hema moja ilikuwa duniani, na nyingine iko mbinguni.TU 197.4

  Hema iliyojengwa na Musa ilijengwa kwa kielelezo kile kile cha ile ya mbinguni. Bwana aliagiza akisema, “Sawasawa na hayo yote nikuonyeshayo, mfano wa maskani na mfano wa vyombo vyako vyote, ndivyo nitakavyofanya” “Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano ulioonyeshwa mlimani” “Hema ya kwanza ilikuwa mfano wa wakati ule ambamo ndani yake sadaka na kafara zilitolewa” patakatifu pake, “mfano wa mambo ya mbinguni”. Makuhani walihudumu. “Kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbingu”. “Kristo hakuingia patakatifu palipotengenezwa kwa mikono ndio mfano wa patakatifu halisi, lakini aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu” Kutoka 25:9-10. Waebrania 9:23; 8:5; 9:24.TU 198.1

  Hekalu la mbinguni ndilo asili ya hema lililojengwa na Musa ikiwa mfano. Uzuri wa hema la duniani ulionyesha mfano wa utukufu wa hekalu la mbinguni mahali ambapo Kristo anahudumu kwa ajili yetu mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ukweli wa hekalu la mbinguni na wokovu wa mwanadamu ulifundishwa hasa kwa huduma zilizofanyika katika hema takatifu la hapa duniani.TU 198.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents