Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kutakaswa kwa Patakatifu

  Utakaso kwa kweli lazima utimizwe kwa damu ya Kristo. “Pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo” Ondoleo au kuweka dhambi mbali ndiyo kazi inayotakiwa kukamilishwa.TU 200.3

  Lakini dhambi na mbingu huhusianaje? Jambo hili litaeleweka kwa kuchunguza huduma iliyokuwa ikifanyika katika patakatifu pa duniani, jinsi makuhani walivyokuwa wakihudumu. Waebrania 8:5.TU 200.4

  Huduma ya patakatifu pa duniani ilikuwa na sehemu mbili. Makuhani walihudumu kila siku katika patakatifu wakati ambapo kuhani mkuu alihudumu mara moja kwa mwaka katika patakatifu mno. Huduma hiyo ya mara moja kwa mwaka iliitwa huduma ya upatanisho, ambayo ilihusu utakaso wa patakatifu. Siku kwa siku mwenye dhambi aliyetubu alileta sadaka yake, akaweka mikono yake juu yake, akaungama makosa yake, ambayo ni sawa anahamisha dhambi zake na kuziweka kwa sadaka hiyo isiyo na hatia. Kisha mnyama huyo wa sadaka alichinjwa. “Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu” Lawi. 17:11. Sheria ya Mungu iliyovunjwa ilidai uhai wa mvunjaji. Damu huwa badala ya uhai wa mwenye dhambi ambaye hatia yake imechukuliwa na yule mnyama wa sadaka. Basi kuhani alichukua damu hiyo mpaka patakatifu akainyunyiza mbele ya pazia, ambalo hukinga sheria ya Mungu iliyovunjwa. Kwa huduma hiyo dhambi ilihamishwa na kuwekwa katika patakatifu. Wakati mwingine damu haikupelekwa katika patakatifu, ila kuhani aliila nyama ya sadaka. Mambo yote mawili, yaani kunyunyiza damu na kula nyama, yalifananisha jambo moja tu, ndiyo kuihamisha hatia kutoka kwa mwenye hatia na kuiweka katika patakatifu. Kazi hiyo iliendelea daima mwaka mzima. Dhambi za Waisraeli zilihamishwa namna hiyo na kuwekwa katika patakatifu, na hiyo ilikuwa kazi ya lazima ya kuhamisha dhambi zao.TU 200.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents