Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  “Haya Bwana Arusi Yuaja”

  Kule kuja kwa Kristo katika patakatifu mno, kama Kuhani Mkuu ili kutakasa patakatifu, (Daniel 8:14) na kule kuja kwa Kristo, yaani Mwana wa Adamu kwa mzee wa siku, (Daniel 7:13) na kule kuja kwa Bwana katika hekalu lake, (Malaki 3:11), yote ni tukio moja tu. Hili pia hufananishwa na kuja kwa Bwana arusi kama inavyoelezwa katika mfano wa wanawali wa Mathayo 25.TU 205.1

  Katika mfano huo, bwana arusi alipokuja, wale waliokuwa tayari waliingia arusini pamoja naye. Kuja huku kwa bwana arusi hutokea kabla ya arusi. Arusi ni mfano wa kukaribishwa na Kristo katika ufalme wake. Mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ambao ndio makao makuu ya ufalme wake huitwa bibi arusi, mke wa mwana Kondoo. Malaika aliwaambia Yohana, “Njoo huku, nitakuonyesha ule mji mkuu, Yerusalemu ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu”. Ufunuo 21:9-10.TU 205.2

  Bibi arusi anafananishwa na Mji Mtakatifu, na wanawali waliokwenda kumlaki Bwana arusi ni mfano wa kanisa. Katika Ufunuo watu wa Mungu wasemwa kuwa ndio wageni katika karamu ya arusi. Kama ni wageni, hawawezi kuwa bibi arusi. Kristo atapokea kutoka kwa Mzee wa siku huko mbinguni, mamlaka na utukufu na ufalme. Yerusalemu mpya, ambao ni makao makuu “ya ufalme wake, umepambwa kama bibi arusi anayepambwa kwa mumewe”. Baada ya kuupokea ufalme, atakuja kama mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana ili kuwaokoa watu wake, ambao watashiriki karamu hiyo ya arusi ya Mwana Kondoo. Daniel 7:14; Ufunuo 21:2.TU 205.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents