Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kufunga kazi Katika Patakatifu

  Katika mfano wa Mathayo 22 hukumu hutangulia arusi. Kabla ya karamu ya arusi kuendeshwa, mfalme aliingia kuona kama wageni wake wote wako sawa; wakiwa na mavazi ya arusi, yaani tabia safi ya kweli iliyooshwa kwa damu ya Mwana Kondo. Ufunuo 7:14. Wote watakao onekana kuwa wanayo mavazi ya arusi, wanakubaliwa ili ashiriki katika ufalme wa Mungu na kuketi katika kiti chake cha enzi. Kazi hii ya kuchunguza tabia za watu ndiyo hukumu ya upelelezi, ambayo ndiyo kazi ya mwisho katika patakatifu pa mbinguni.TU 206.3

  Mambo yote ya watu waliojiita kuwa wakristo tangu vizazi vyote, yatakapokuwa yamekwisha kuchunguzwa na kuamuliwa, ndipo wakati wa rehema na mlango wa rehema utafungwa. Ndipo kwa kifupi ni kwamba, “Na wale waliokuwa tayari kuingia pamoja naye arusini, mlango ukafungwa. Hapo tunapelekwa moja kwa moja mpaka mwisho wa kazi ya kushughulikia wokovu wa mwanadamu. Huo ndio mpango mkuu wa wokovu.”TU 206.4

  Katika patakatifu pa duniani, siku ya upatanisho, wakati kuhani mkuu alipoingia katika patakatifu mno, huduma katika chumba cha kwanza cha patakatifu zilikoma. Hali kadhalika Kristo naye alipoingia katika patakatifu mno huko mbinguni ili kukamilisha kazi ya ukombozi, huduma katika chumba cha kwanza ilikoma. Halafu kazi katika chumba cha pili, yaani patakatifu mno; ilianza. Kristo alikuwa amemaliza sehemu moja ya kazi yake ya ukombozi, ndipo alianza sehemu ya pili ya kazi. Bado angali akiombea kwa Baba damu yake iwatakase wenye dhambi.TU 206.5

  Jinsi ukweli ulivyo kwamba mlango wa tumaini rehema ambao kwa miaka 1844 ulikuwa wazi, ulivyokuwa ukifungwa, mlango mwingine ulikuwa ukifunguliwa. Msamaha wa dhambi ulikuwa ukitolewa kwa maombezi ya Kristo katika patakatifu mno. Bado kulikuwa na mlango wazi katika patakatifu pa mbinguni, ambako Kristo anawahudumia wenye dhambi.TU 207.1

  Sasa itadhihirika maana ya maneno ya Kristo katika Ufunuo yaliyosemwa hasa kwa wakati huu: “Haya ndiyo anenayo yeye aliye Mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunguaye wala hapana afungaye. ‘…Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hakuna awezaye kuufunga’”. Ufunuo 3:7-8.TU 207.2

  Wale wanaofuatana na Kristo katika kazi yake ya uombezi watafaidika na kupata ukombozi, ambapo wale wasiojali nuru wanayofunuliwa hawatapata lolote. Wayahudi waliokataa kumwamini Kristo kuwa Mwokozi wao hawakuweza kupata msamaha kwake. Wakati Yesu alipopaa mbinguni na kuwamwagia wafuasi wake karama yake, Wayahudi waliachwa wakitangatanga gizani huku wakiendelea kutoa dhabihu za wanyama na sadaka ambazo ni za kazi bure. Mlango ambao watu waliingia kwa Mungu kwa njia ya dhabihu za wanyama ulikuwa umefungwa. Wayahudi walikataa kumtafuta yeye ambaye ndiye mlango, naye angepatikana katika patakatifu pa mbinguni.TU 207.3

  Wayahudi hao wasioamini waliweka kielelezo cha kutojali na kutoamini kati ya wakristo wengi ambao hujipumbaza wenyewe wasishughulike kujua kazi ya Kuhani wetu mkuu. Katika mfano wa huduma ya kuhani hapa duniani, Kuhani mkuu alipoingia katika patakatifu mno, Waisraeli wote walitakiwa kukusanyika na kuzunguka patakatifu, huku wakijinyenyekeza mbele za Mungu kwa mioyo yao yote, ili wapate msamaha wa dhambi zao, wasije wakakatiliwa mbali na kusanyiko la watakatifu. Je, ni muhimu kiasi gani kwa huduma ya Kuhani wetu Mkuu sasa ambayo ni kama siku ya upatanisho, jinsi inavyotupasa kuelewa wajibu unaotupasa?TU 207.4

  Ujumbe ulitumwa kutoka mbinguni kuja ulimwenguni wakati wa Nuhu. Wokovu wao ulitegemea jinsi walivyojali ujumbe huo. Mwanzo 6:6-9; Waebrania 11:7. Wakati wa siku za Sodoma ilikuwa ni Luthu na mkewe na binti zake wawili tu, ndio wangepona, na wengine wote waliangamizwa na moto ulitoka mbinguni. Mwa. 19. Hali kadhalika siku za Kristo. Mwana wa Mungu aliwahubiria Wayahudi wasiojali, akasema, “Nyumba yenu mmeachiwa ukiwa”. Mathayo 23:38. Akaingia siku za mwisho, mwokozi alisema, “Wala hawakuipenda ile kweli ili waokoke. Kwa hiyo Mungu atawaletea nguvu ya upotevu ili wauamini uongo”. 2Thes. 2:10-11. Kwa vile wasivyojali neno Lake wala mafundisho yake, Mungu atawaondolea Roho Yake, na kuwaacha waamini uongo ambao wanaupenda. Lakini Kristo bado anawaombea wanadamu, na nuru itatolewa kwa wale wanaoitafuta.TU 207.5

  Kupita kwa wakati katika 1844 kulifuatiwa na kipindi kigumu cha majaribu mazito kwa wale walioshikilia imani ya marejeo. Nafuu yao ilikuja tu kwa nuru iliyowaongoza waone umuhimu wa huduma ya patakatifu pa mbinguni. Walipongojea na kuomba waliona kuwa Kuhani wetu Mkuu ameingia katika patakatifu mno ili kuanza kazi ya sehemu ya pili. Wakimfuata kiroho kwa imani, waliongozwa pia kuona kufungwa kwa kazi ya kanisa. Walifahamu kwa dhahiri ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili, nao walijitayarisha kupokea na kutangaza ulimwenguni onyo kuu la ujumbe wa malaika wa tatu wa Ufunuo 14.TU 208.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents