Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwito Kumwabudu Mwumbaji

  Wajibu wa kumwabudu Mungu unahusika kwa kuwa yeye ni Mwumbaji. “Njooni tuabudu tusujudu, tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba” Zaburi 95:6; 96:5; 100:3; Isaya 40:25, 26; 45:18.TU 210.4

  Katika ufunuo 14 watu wanaitwa ili kumwabudu na kumsujudu Mwumbaji na kushika amri zake. Mojawapo ya amri hizi humwonyesha Mungu kuwa ni Mwumbaji. “Siku ya saba ni sabato ya Bwana Mungu wako …. Maana kwa siku sita Bwana alizifanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo, akapumzika siku ya saba akaitakasa”. Kutoka 20:10-11. Bwana asema, “Sabato ni ishara …. Mpate kujua kuwa mimi ni Bwana Mungu wenu”. Ezekieli 20:20. Kama sabato ingeshikwa na watu wote wa ulimwengu, watu wangeelekeza ibada zao kwa Mungu. Pasingalikuwako mtu yeyote aabuduye sanamu, kafiri wala asiyeamini. Kushika Sabato ni ishara ya uaminifu na utii kwa yule aliyeumba mbingu na nchi, na bahari, na chemichemi za maji. “Ujumbe unaowaita watu kumwabudu Mungu na kushika amri zake, hasa huwaita washike amri ya nne, yaani Sabato.”TU 211.1

  Mbali na wale washikao amri za Mungu na kuwa na imani ya Yesu, ujumbe wa malaika wa tatu huonyesha kundi jingine la watu; “Mtu yeyote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo wa ghadhabu ya Mungu”. Ufunuo 14:9-10. Ni nini kinachomaanishwa na mnyama, sanamu au chapa?TU 211.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents