Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uthibitisho wa Joka

  Unabii ambao mifano hii inatajwa unapatikana tangu katika Ufunuo 12. Joka lililotaka kumharibu Kristo wakati wa kuzaliwa kwake, yasemekana kuwa ni Shetani (Ufunuo 12:9) alimchochea Herode amwangamize Mwokozi. Lakini mjumbe wa Shetani katika kupingana na Kristo na watu wake katika karne ya kwanza, ilikuwa ni serikali ya Rumi, ambamo ukafiri ulistawi ndani yake kama dini. Kwa hiyo joka kwa upande wa pili ni Rumi ya kikafiri.TU 211.3

  Katika Ufunuo 13 kunatajwa mnyama mwingine, “afananaye na chui” ambaye joka alimpa “nguvu zake” “na kiti chake cha enzi, na uwezo mwingi”. Mfano huu kama unavyokubaliwa na Waprotestanti wengi, ni mfano wa upapa; ambao ulishika utawala uliokuwa ukiendeshwa na serikali ya Rumi. Ule mfano wa Chui unaonekana kuwa; “apewa kinywa chenye kunena maneno makuu ya kufuru… akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na masikani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila jamaa na lugha.” Ufunuo 13:2, 5-7. Unabii huu ambao karibu ufanane na ule wa Danieli 7 wa pembe ndogo, bila shaka unaeleza habari za Upapa wa Rumi.TU 211.4

  Walimpa uwezo wa kufanya kazi yake “miezi arobaini na miwili”- Miaka mitatu na nusu au siku 1260 za Daniel 7, wakati ambao uwezo wa papa utawatesa watu wa Mungu. Muda huu kama unavyoelezwa katika sura zilizopita ulianzia na uwezo wa upapa katika A.D 538 mpaka ukamalizika mwaka 1798. Wakati huo ndipo uwezo wa upapa ulipopata pigo la mauti, na utabiri ukatimia kwamba; “Mtu akichukua mateka atachukuliwa mateka.”TU 212.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents