Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuinuka kwa Uwezo Mpya

  Wakati huu mfano mwingine uliletwa. “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwanakondoo” Ufunuo 13:11. Taifa hili halifanani na mataifa yaliyoelekezwa katika sura zilizotangulia, yaani mifano iliyoendelezwa hapo mwanzoni. Mataifa makuu yaliyoutawala ulimwengu yalielezwa katika unabii wa Danieli kuwa kama wanyama wakubwa wa mawindo, waliotokea katika bahari kuu, wakati “pepo za mbinguni zilipovuma juu yake” Daniel 7:2. Katika Ufunuo 17:15 malaika alielekeza kwamba yale maji uliyoyaona ni jamaa na makutano na mataifa na lugha. Upepo au dhoruba ni mapambano au alama ya vita. Pepo nne zishindanazo juu ya bahari ni mapambano ya kutisha ya ushindi na mapinduzi ambayo falme zimejipatia utawala.TU 212.2

  Lakini mnyama aliye na pembe zifananazo na za mwanakondoo alionekana akiinuka “kutoka katika nchi” Badala ya kushinda utawala mwingine ili yeye apate kutawala, taifa linaloelezwa kwa mfano huu liliinuka katika nchi ambayo haikuwa na watu. Taifa hilo lilistawi katika amani na utulivu. Taifa hili lazima litafutwe katika bara la magharibi.TU 212.3

  Katika mwaka 1798 ni taifa gani lililoinuka na kustawi likawa na nguvu, ambalo lilivuta macho ya ulimwengu mzima kuelekea? Ni taifa moja tu, moja peke yake, ndilo linalopatana na unabii huu — yaani Marekani (United States of America). Maneno ya Maandiko Matakatifu ndiyo yamelieleza taifa hili karibu na kila kitu bila kasoro; jinsi kuinuka kwake kutakavyokuwa. Mwandishi fulani mashuhuri akiandika siri ya kuinuka kwa taifa hilo kutoka mahali pasipokuwa na watu, asema, “Tumekuwa taifa kuu, katika hali ya ukimya sawa kama mbegu inavyokuwa kimya kimya”. Gazeti la Ulaya, likiandika habari za Marekani katika mwaka 1850, lilisema, “Marekani imezuka kimya kimya” “kila siku huongezeka kuwa maarufu” kwa uwezo na kiburi.TU 212.4

  “Ana pembe mbili kama mwanakondoo”.TU 212.5

  Pembe kama mwanakondoo, huonyesha hali ya ujana, bila madhara, na hali ya uungwana. Baina ya wakristo waliokimbilia Marekani mara ya kwanza, kutoka katika mateso ya Ulaya na shuruti za dini, wengi waliazimu kuwa na uhuru wa dini, na uhuru wa utu binafsi. Tangazo la kujitawala lilifafanua kuwa, “watu wote waliumbwa sawa, wakapewa haki ya uhuru wa kila mtu, kujiamulia mambo yanayomhusu yeye binafsi, kama maisha anayotaka kuishi, uhuru bila kutegemea mtu mwingine amwamulie mambo yake, na kufuata furaha yake. Katiba ya kujitawala iliweka wazi mambo hayo ya kila mtu kufuata matakwa yake. Kwamba utawala hautakuwa katika mikono ya mtu mmoja, ila utakuwa katika mikono ya wajumbe wanaowakilisha watu. Uhuru wa dini uliotolewa, kuwa kila mtu afuate dini anayopenda, sio kulazimisha. Serikali na Uprotestanti vikawa ndiyo msingi wa taifa hilo. Hivyo ndio ilikuwa siri ya kustawi na kufanikiwa kwa taifa. Mamilioni ya watu wamehamia huko, na Marekani imekuwa mojawapo ya mataifa makuu yenye nguvu kabisa na ustawi wa ajabu duniani.TU 213.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents