Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mnyama na Sanamu Yake

  “Mnyama wa pembe mbili kama mwanakondoo aliwaamuru wote, wadogo kwa wakubwa matajiri kwa maskini, walio huru kwa watumwa, wapokee alama ya mnyama katika mkono wake wa kuume au vipaji vya nyuso zao ya jina lake” Ufunuo 13:16-17. Malaika wa tatu hutoa onyo kuwa “Mtu awaye yote akimsujudia huyo mnyama na sanamu yake, na kupokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo wa ghadabu ya Mungu”.TU 215.2

  “Mnyama” ambaye ibada yake inalazimishwa ni yule mnyama chui, wa ufunuo 13, yaani papa. Sanamu ya mnyama inamaanisha Uprotestanti uliopotoka ambao wakati makanisa ya Kiprotestanti yatakapotafuta msaada wa serikali ili kutekeleza mambo ya kanisa, watafikia kipeo. Alama ya mnyama bado haijatekelezwa.TU 215.3

  Wale washikao amri za Mungu watatofautiana na wale waabuduo mnyama na sanamu yake, na kupokea chapa yake. Kushika sheria ya Mungu, kwa upande mmoja; na kuivunja kwa upande mwingine, kutapambanua baina ya wamwabuduo Mungu, na wamwabuduo mnyama.TU 215.4

  Tabia maalum ya mnyama na sanamu yake ni kuvunja amri za Mungu. Daniel asema Kuhusu pembe ndogo, yaani upapa, “Naye ataazimu kubadili majira na sheria” Daniel 7:25. Paulo naye anena kuhusu uwezo huo huo. “mtu wa kuasi” (2Thes. 2:3) ajiinuaye juu ya Mungu. Kule kubadili amri za Mungu ndilo jambo la kujiinua juu ya Mungu ambalo papa ametenda. Mtu yeyote anayeendelea kushika amri hizo jinsi zilivyobadilishwa, huwa anatoa heshima yake kwa papa, na sheria ya papa.TU 215.5

  Hivyo ndivyo alama ya utii kwa papa, na wala sio kwa Mungu.TU 216.1

  Mapapa wamejaribu kubadili sheria ya Mungu. Amri ya nne, yaani Sabato, imebadilishwa na kuweka siku ya kwanza badala yake, na watu wanaishika badala ya Sabato ya siku ya saba. Badiliko hilo limefanywa kwa makusudi kabisa. “ataazimu kubadili majira na sheria” Kubadili amri ya nne ya amri za Mungu, hutimiza kabisa unabii. Hapo ndipo uwezo wa papa hujiinua dhahiri juu ya Mungu.TU 216.2

  Wanaomwabudu Mungu watajulikana wazi kwa vile vile watakavyoishika amri ya nne, yaani Sabato, ambayo ni ishara ya uwezo wake wa kuumba. Wanaoabudu mnyama watajulikana kwa juhudi yao ya kuharibu ukumbusho wa uwezo wa Mungu wa kuumba; nao wataiheshimu siku iliyowekwa na kanisa la Rumi. Ilikuwa kule kushika Jumapili kama siku ya Bwana, ndipo papa aliitetea na kudai kwa kiburi kuwa siku hiyo iheshimiwe na watu wote. Lakini Biblia inasema kuwa siku ya saba ndiyo Sabato ya Bwana. Kristo alisema, “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato” Marko 2:28. Soma pia Isaya 58:13; Mathayo 5:17-19. Madai yanayodaiwa na watu kuwa Kristo alibadili Sabato ni uongo, yanakanushwa na yeye mwenyewe.TU 216.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents