Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kimya Kabisa Katika Agano Jipya

  Waprotestanti wanakiri kabisa kuwa katika Agano Jipya hakuna neno lo lote linalotaja kuwa amri ya nne, yaani sabato imeondolewa, wala neno la kushika Jumapilli kama siku takatifu ya kuabudu.TU 216.4

  Mpaka wakati Kristo alipokufa msalabani, hapakuwako badiliko lolote kuhusu siku, kama maandiko yasemavyo. Mitume hawakubadili chochote kuhusu kuondoka sabato ya siku ya saba, na kuweka siku ya kwanza badala yake.TU 216.5

  Kanisa la Rumi linakiri kuwa wao ndio walibadili sabato, na kusema kuwa Waporotestanti wanapokubali kushika siku ya Jumapili kama siku ya ibada, wanayatambua mamlaka yao. Wao husema: “Sheria ya zamani, yaani sabato, ndiyo iliyotakaswa; lakini kanisa letu likiagizwa na Yesu na Roho wa Mungu, limebadili sabato ya Jumamosi na kuweka Jumapili badala yake. Sasa tunatakasa siku ya kwanza, wala sio siku ya saba. Hivyo sasa Jumapili ndiyo siku ya Bwana”TU 216.6

  Ili kuonyesha uwezo au mamlaka yao, wafuasi wa Rumi huandika kwamba kule kubadili sabato na kwenda jumapili badala yake, ambavyo hata Waprotestanti wanakubali kushika, huonyesha uwezo wa kanisa kuamuru sikukuu na kuamuru ushikaji wake chini ya dhambi.TU 216.7

  Basi kubadili sabato kuna maana gani basi, isipokuwa kuonyesha uwezo au alama ya mamlaka ya kanisa la Rumi? Hivyo ndivyo “alama ya mnyama”TU 217.1

  Kanisa la Rumi halijaacha madai yake ya ukuu. Ulimwengu na makanisa ya Kiprotestanti wanapokubaliana na sabato bandia iliyowekwa na Rumi, na kukataa sabato ya Biblia, hukiri kuwa kanisa la Rumi lina uwezo kamili. Kwa kufanya hivyo wanapuuza kanuni zile zilizowatenganisha na Warumi, ambazo husema, “Biblia na Biblia tu, ndiyo dini ya Waprotestanti” Kwa kadri msukumo wa Jumapili unavyozidi kusonga mbele, na kuungwa mkono na wengi, baadaye makanisa yote ya Kiprotestanti yatajikuta yako chini ya bendera ya Rumi.TU 217.2

  Warumi husema kuwa kule kushika jumapili kwa Waprotestanti huonyesha kuwa wanaheshimu Rumi na kukubaliana nayo. Kutaka msaada wa serikali ili kulazimisha watu washike Jumapili kutafanya sanamu kwa mnyama. Hivyo basi amri ya jumapili katika Marekani itakuwa amri ya kuabudu mnyama na sanamu yake.TU 217.3

  Wakristo wa zamani walishika jumapili wakidhani kuwa walikuwa wakishika sabato ya Biblia, na bado jumapili iliwekwa na Mungu. Watu hao Mungu hupokea ibada zao na uaminifu wao. Lakini wakati amri ya jumapili itakapowekwa kisheria, ulimwengu utaangazwa na kuiona sabato ya kweli, ndipo hapo wale watakaoasi amri ya Mungu na kuendelea kushika jumapili iliyowekwa na Rumi, watakuwa wanaheshimu Rumi badala ya Mungu. Watakuwa wanamwabudu mnyama na sanamu yake. Basi watakuwa wanaipokea ishara ya Rumi — yaani alama ya mnyama. Bado mpaka amri ya jumapili itakapowekwa, ndipo watu watachagua kati ya kumtii Mungu au mwanadamu, na wale watakaoendelea kumwasi Mungu watapokea “alama ya mnyama”.TU 217.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents