Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  26/Mashujaa wa Kutetea Kweli

  Matengenezo ya Sabato katika siku za mwisho yalitabiriwa katika Isaya “Bwana asema hivi, shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu u karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa. Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuia mkono wake usifanye uovu wowote. Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asivunje, na kulishika sana agano langu; Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala” Isaya 56:1-2,6-7.TU 219.1

  Maneno haya yanahusu ukristo. Kama inavyoonyesha kwenye fungu la nane. Hapa ni kivuli cha mkusanyo wa mataifa kwa njia ya Injili kinavyoonyeshwa, wakati watumishi wa Mungu watakapotawanyika duniani kuhubiri habari njema.TU 219.2

  Bwana anaamuru akisema, “Ufunge huo ushuhuda, ukatie muhuri sheria kati ya wanafunzi wangu” Isaya 8:16. Mhuri wa sheria ya Mungu unapatikana katika amri ya nne. Ni amri hii pekee yake kati ya hizo kumi inayotaja jina na cheo cha mtoa sheria. Sabato ilipobadilishwa na mapapa, muhuri iliondolewa kutoka kwenye sheria. Wanafunzi wa Yesu wanatakiwa waurudishe muhuri huo kwa njia ya kuitunza sabato kama ukumbusho wa Mwumbaji na alama ya uwezo wake.TU 219.3

  Agizo linatolewa likisema, “Piga kelele usiache, paza sauti kama tarumbeta, uwahubiri watu wangu kosa lao. Watu ambao Bwana huwaita, ‘Watu wangu’, lazima waonyeshwe uasi wao, ambao hujiona kuwa wenye haki katika kumtumikia Mungu. Lakini makemeo ya kutisha na maonyesho yanapotolewa na mchunguza mioyo hujikuta kuwa wanavunja sheria ya Mungu”. Usata 58:1-2,TU 219.4

  Nabii huonyesha sheria ambayo imeachwa bila kujaliwa. “Utainua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa mwenye kutengeneza mahali palipobomoka, na mwenye kurejeza njia za kukalia. Kama ukigeuza mguu wako usiihalifu Sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu yenye heshima; ukitukuza kwa kutozifanya njia zako mwenyewe, na wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika Bwana” Isaya 58:12-14.TU 219.5

  Mabomoko yaliyofanywa katika sheria ya Mungu wakati Sabato ilipobadilishwa, na uwezo wa mapapa. Lakini wakati umefika ambapo lazima kuziba mabomoko hayo.TU 219.6

  Sabato ilishikwa na Adamu katika bustani ya Edeni alipokuwa hajaanguka, tena aliendelea kuishika hata alipokuwa ameanguka na kutubu, akiwa amefukuzwa katika bustani. Ilishikwa na wazee wote, tangu Habili mpaka Nuhu, Ibrahimu, mpaka Yakobo. Bwana alipowaokoa watu kutoka Misri, aliitangaza Sabato mbele ya makutano, pamoja na sheria nzima.TU 220.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents