Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Siyo Mapenzi ya Mungu

  Hayakuwa mapenzi ya Mungu kwamba Waisraeli watangetange jangwani miaka arobaini. Alikuwa na nia ya kuwaongoza moja kwa moja mpaka Kanaani na kuwamilikisha huko, wakiwa watakatifu wenye furaha. Lakini, “hawakuweza kuingia huko kwa ajili ya kutokuamini kwao” Waebrania 3:19. Vivyo hivyo hayakuwa mapenzi ya Mungu kwamba Kristo angekawia kurudi namna hiyo, na watu wake wazidi kukaa katika dunia hii yenye dhambi na huzuni kwa miaka mingi. Kutokuamini kwao kuliwatenga na Mungu. Kwa ajili ya kuuhurumia ulimwengu, Yesu amekawiza kurudi kwake, ili wenye dhambi wasikie maonyo na kutafuta mahali pa kukimbilia, wakati ghadhabu ya Mungu itakapomwagwa duniani.TU 221.3

  Sasa, kama wakati wa zamani, utangazaji wa ujumbe wa Mungu utakabiliwa na mapingamizi. Wengi wanaoutetea ukweli na kupinga imani ya wengi. Eliya aliitwa kuwa “msumbua Israeli; Yeremia akaitwa kwamba ni msaliti” Paulo akaitwa kuwa “mchafua hekalu” Tangu wakati huo mpaka sasa, wale wanaoitetea kweli wameonewa kuwa mahaini, wazushi, wenye faraka.TU 221.4

  Ungamo la imani ya wakatatifu wa kale, na wafia dini, ambayo ni vielelezo vya ushujaa wa ukweli huwatia moyo wale walioitwa kuwa mashahidi wa Mungu. Agizo kwa mtumishi wa Mungu kwa wakati huu: “Paza sauti yako kama tarumbera, uwaonyeshe watu wangu makosa yao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao”. “Nimekuweka uwe mlinzi wa nyumba ya Israeli; kwa hiyo sikia neno langu, ukawape watu maonyo yangu”. Isaya 58:1; Eze. 33:7.TU 222.1

  Pingamizi kubwa la kuzuia watu wasiukubali ukweli ni kwa sababu huwaingilia katika furaha zao na kuwakemea. Huu ndio ubishi tu wa kutoipokea kweli. Lakini wafuasi wa kweli wa Mungu, hawangojei ukweli upendwe na kuamini na watu wote. Wanaukubali msalaba, kama Paulo asemavyo: “Maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya muda kitambo tu yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana” Na tena, “akahesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri” 2Kor. 4:26; Waebrania 11:26.TU 222.2

  Yatupasa kuchagua haki kwa kuwa ni haki; na kumwachia Mungu mengine yote. Mtu ashikaye kanuni, mwenye imani, aliye jasiri, ndiye ahitajikaye ulimwenguni ili alete matengenezo. Mtu, au watu wa namna hiyo ndiyo wanaotakiwa wafanye matengenezo kwa wakati huu na kuyaendeleza.TU 222.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents