Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ni kweli Imani Peke Yake

  Kazi hii inaweza kukamilika kwa imani peke yake, katika uwezo wa Roho Mtakatifu akaaye ndani ya mtu. Mkristo atasikia hali ya dhambi ikimkabili, lakini atapata uwezo wa kushidana nayo. Hapo ndipo msaada wa Kristo unapohitajika. Udhaifu wa kibinadamu unapounganika na uwezo wa kimbingu, ndipo imani husema, “Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.” 1Kor. 15:57TU 227.3

  Kazi ya utakaso ni ya maendeleo. Mwenye dhambi anapotubu na kupata kibali cha Mungu, hapo ndipo maisha ya ukristo huanza. Sasa yapasa aendelee mpaka ukamilifu, kukua hata kimo cha utimilifu wa Kristo. “Nakaza mwendo niifikie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.” Waebrania 11:6; Waefeso 4:13; Wafilipi 3:14.TU 227.4

  Watu ambao wanapata utakaso wa Biblia, wataonyesha hali ya unyenyekevu. Huona upungufu wao, wanapojilinganisha na ukamilifu wa Mungu. Nabii Daniel alikuwa kielelezo kizuri kuhusu utakaso. Badala ya kujidai kuwa mtu safi na mtakatifu, nabii mkuu huyu alijiweka pamoja na wenye dhambi wengine wa Israeli wakati alipokuwa akiomba kwa ajili ya watu wake. Daniel 10:11; 9:15,18,20: 10:8,11.TU 227.5

  Kwa wale wanaotembea chini ya kivuli cha msalaba wa Kalvari, hapata kuwako kujitukuza, wala kujivuna kuwa hawana dhambi. Hujisikia daima kuwa dhambi zao ndizo zilizosababisha mateso ya Mwana wa Mungu, kwa kuwa na mawazo hayo watakuwa na fedhaha tu. Wale wanaoishi karibu na Kristo wanapambanua hali ya unyonge na uovu wa wanadamu, na huona kuwa tumaini lao ni kwa mwokozi aliyesulubiwa na kufufuka ufuni.TU 228.1

  Utakaso unaoonekana katika ulimwengu wa kidini sana, ambao ni wa majivuno bila kujali sheria ya Mungu ni mgeni kwa Biblia. Hufundisha kuwa utakaso huo ni wa kitambo tu, bora uwe na imani, basi unapata mara moja bila kungoja. Bora uamini, tu utaupata utakatifu kamili. Hakuna juhudi yoyote inayohitajika ili kuupata, ni kuamini tu. Watu hujidai kuwa wamepata utakatifu, na kwa wakati ule ule wanakana uwezo wa mamlaka ya sheria ya Mungu, wakisema kuwa wamewekwa huru kutokana na kushika sheria. Lakini je, inawezekana kufikia hali ya utakatifu bila kufikiana na kanuni za utakatifu, ambazo huoyesha mapenzi ya Mungu?TU 228.2

  Ushuhuda wa neno la Mungu hukanusha mafundisho mapotofu ya jinsi hiyo ya imani bila matendo. Siyo imani ya peke yake yenye kufikia matakwa ya mbinguni, bila kuwa na masharti ambayo kwayo rehema hupatikana. Huo ni ufedhuli mtupu. Yakobo 2:14-24.TU 228.3

  Watu wasijidanganye kuwa wanaweza kufikia utakatifu wakati wanapozivunja sheria za Mungu kwa makusudi. Dhambi inayojulikana hunyamazisha sauti ya Roho wa Mungu anayeshuhudia katika mioyo ya watu, nayo humtenganisha mtu na Mungu. Ijapokuwa Yohana anaeleza kabisa habari za upendo, hakusita kutaja tabia ya watu ambao hujidai kuwa wametakaswa na kwa wakati ule ule wanaziasi amri za Mungu.TU 228.4

  “Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, hakika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli” 1 Yoh. 2:4-5. Hiki ndicho kipimo cha uchaji wa Mungu. Kama wakizihafifisha amri za Mungu au wakivunja mojawapo ya amri zake na kuwafundisha watu hivyo (Mathayo 5:18-19) tutajua ya kuwa madai yao hayana msingi.TU 228.5

  Wale wanaojidai kuwa hawana dhambi ni dhahiri kuwa wako mbali na utakatifu. Mtu wa jinsi hiyo hana ule uongofu wa kweli, wala hajui utakatifu wa Mungu ulivyo na hana habari na jinsi dhambi ilivyo mbaya mno. Kiasi anavyokuwa mbali sana na Kristo, ndivyo anavyojiona kuwa mtakatifu yeye mwenyewe.TU 228.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents