Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Utakaso wa Biblia

  Utakaso kuhusu mtu mzima, yaani roho, dhamiri na mwili. Soma 1Thes. 5:23. Wakristo wanaagizwa kutoa miili yao kuwa dhabihu iliyo hai, takatifu, inayokubalika mbele za Mungu Rum. 12:1. Kila kitendo kinachoudhoofisha mwili au akili, humfanya mtu asifae kufanya huduma ya Mwumbaji wake. Wote wanaompenda Mungu kwa mioyo yao yote daima watatafuta kuhusianisha viungo vyao na nguvu zao wapate kuzitii amri za Mungu, na kufanya mapenzi yake. Hawatajichafua au kujinajisisha kwa hali yo yote mpaka wakuwa hawafai kutoa dhabihu ya miili yao kuwa takatifu, kwa Baba yao wa mbinguni.TU 229.1

  Kila kitendo cha dhambi au cha tamaa ya mwili au chakula huelekea kudhoofisha uwezo wa akili ya utambuzi. Neno la Mungu, au Roho wa Mungu huwa na mvuto kidogo tu kwa mtu wa namna hiyo. Na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu 2kor. 7:1.TU 229.2

  Ni wakristo wangapi ambao hujinajisisha wenyewe kwa njia ya ulafi, ulevi na anasa haramu. Kanisa mara nyingi huunga mkono maovu kwa njia ya kujaza urembo na madoido ya kila namna, ambayo hunyang'anya, upendo wa Kristo katika mioyo yao. Je, kama yesu angaliingia katika makanisa ya leo na kuona mambo ya kianasa yaliyomo, ambayo yanatajwa kwa jina la dini asingaliwafukuza, kama alivyowafukuza wale wabadili fedha hekaluni zamani?TU 229.3

  “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu” 1Kor. 6:19-20. Mtu ambaye mwili wake ni hekalu la Roho Mtakatifu, hawezi kujitia utumwani kwa njia ya kufanya mazoezi ya ufedhuli. Uwezo wake ni mali ya Kristo. Mali yake yote ni mali ya Bwana. Basi anawezaje kuharibu mali hiyo?TU 229.4

  Wakristo hugharimia fedha nyingi kwa mwaka kwa ajili ya mambo ya anasa. Mungu hunyang'anywa zaka na sadaka, wakati matumizi ya anasa huchukua sehemu kubwa ya mali yao, zaidi kuliko wanayotoa kwa ajili ya kusaidia masikini na kwa kueneza Injili. Kama wote wanaojiita kuwa ni Wakristo wangekuwa waaminifu katika kutumia mali zao, badala ya kuzitumia ovyo, wakaziweka katika hazina ya mbinguni, wangekuwa mfano mzuri wa kiasi na kujinyima. Ndipo wangekuwa nuru ya ulimwengu.TU 229.5

  Tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima (1Yoh. 2:16) huwatawala watu maelfu na maelfu. Lakini wafuasi wa Kristo wanao mwito mtakatifu. “Tokeni kati yao mkatengwe nao asema Bwana, msiguse kitu cho chote kilicho kichafu” kwa wale wanaoafikiana na masharti haya, ahadi ya Mungu kwao ni hii, “Nami nitawakaribisha, nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike” 2Kor. 6:17-18.TU 230.1

  Kila hatua ya imani na utii, humleta mtu katika kuunganika na Nuru ya ulimwengu. Nuru kamili za jua la haki huwamulikia watumishi wa Mungu, nao huwangazia wengine. Nyota hutuambia kuwa kuna nuru huko mbinguni ambayo utukufu wake huzingarisha. Hali kadhalila wakristo huudhihirishia ulimwengu kuwa yuko Mungu atawalaye, ambaye anastahili kutukuzwa na kuheshimiwa. Utakatifu wa tabia yake utadhihirika kwa watumishi wake ambao ni mashahidi wake.TU 230.2

  Kwa fadhili zake Kristo tunapta njia ya kufikia kiti cha enzi cha Mungu, mwenye uwezo. “Yeye asiyemwachilia mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia mambo yote bure?” Yesu asema, “Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je, Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa roho Mtakatifu hao wamwombao? Mkiomba lo lote kwa jina langu hilo nitalifanya” “Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu iwe timilifu” Rum. 8:32; Luka 11:13; Yoh. 14:14; 16:24.TU 230.3

  Ni jukumu la kila mtu kuishi maisha yanayotambulika kwa Mungu ili apate baraka zake. Siyo mapenzi ya Baba wa mbinguni kwamba sisi tuishi gizani katika hali ya kutangatanga na kuhukumiwa. Hakuna ushahidi wo wote kwamba unyenyekevu humfanya mtu atembee akiinama chini na kuliwazwa na mawazo ya ubinafsi. Twapaswa kumwendea Yesu na kutakaswa na kusimama mbele ya sheria bila hofu wala waa.TU 230.4

  Wana wa Adamu walioanguka wanaweza kuwa wana wa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Yeye haoni haya kuwaita ndugu zake. Maisha ya ukristo yapasa yawe maisha ya imani, ya ushindi na ya furaha katika Bwana Mungu. “Furaha ya Bwana ndiyo nguvu yenu” “Furahini siku zote” “Ombeni bila kukoma Shukuruni kwa mambo yote, maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu” Ebr. 2:11; Neh. 8:10; 1Tes. 5:16-18.TU 230.5

  Hayo ndiyo matunda ya uongofu wa Kibiblia na utakaso. Kwa kuwa kanuni kuu za sheria kama zilivyowekwa na Biblia, hazifuatwi ndiyo sababu ya hali hafifu makanisani. Hii ndiyo sababu mwamko wa kiroho ni mdogo sana, wala haufuatani na ule wa watu wa zamani wa matengenezo. Ni kwa kutazama tu ndipo tunabadilika. Kanuni zile takatifu zionyeshazo tabia ya Mungu zisipojaliwa, na watu wakitia nia zao kwa hadithi za kibinadamu matokeo yake ni hali ya mauti ionekanayo katika kanisa, yaani kanisa mtu. Ni wakati sheria ya Mungu inapoheshimiwa ipasavyo ndipo mwamko wa kiroho unapoambatana na imani ya kweli ya uongofu halisi vitaonekana katika maisha ya wakristo.TU 230.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents